Connect with us

Album Mpya ya Hakuna Kama Wewe ya Rose Mollel Chipe Kuzinduliwa Tarehe 02.07.2017

Uncategorized

Album Mpya ya Hakuna Kama Wewe ya Rose Mollel Chipe Kuzinduliwa Tarehe 02.07.2017

Kutoka jijini Arusha Tanzania muimbaji mpya wa nyimbo za Injili anayefahamika kwa jina la Rose Mollel (Chipe) anatarajia kuweka wakfu na kuachia album zake mpya mbili ambapo moja inabeba jina la Hakuna Kama Wewe ikiwa katika mfumo wa DVD na nyingine itakuwa kwenye mfumo wa Audio CD ambapo album zote hizi zitazinduliwa rasmi Tarehe 02.07.2017 katika kanisa la KKKT KIRANYI, Barabara ya silentini, Sakina kuanzia saa kumi na mbili na nusu asubuhi mpaka saa tatu asubuhi.

Akiongea na timu ya gospomedia.com muimbaji Rose Mollel (Chipe) amesema kuwa uzinduzi huo pia utaambatana na Tamasha kubwa la kusifu na kuabudu kuanzia saa sita kamili mchana na kusindikizwa na waimbaji mbalimbali kama vile Upendo Nkone, Lembo Junior, Machalii wa Yesu, Shadrack Robert, Baraka Massa, God’s Surrender, Angelina Francis, Upendo Mbila, Kwaya ya Kiinjilisti Kiranyi, Kwaya ya Habari Njema, Kwaya ya Amkeni Azimio, Daniel Ikoja, Upendo Kwaya na Ombeni Kwaya, na msherehashaji katika tukio hilo atakuwa ni Mc Elisha Mashauri.

Rose Mollel (Chipe) pia ameongeza kuwa atabarikiwa sana kuona kila mmoja anafika siku hiyo hasa kwa wakazi wa Arusha na mikoa yote ya jirani ambapo anaamini uzinduzi huo utakuwa baraka kwa kila mmoja atayefika siku hiyo hivyo amesisitiza watu wote kufika siku hiyo na kwa wale ambao watashindwa kufika siku hiyo, baada ya uzinduzi huu album hizo zitaweza kuwafikia watu wote kuanzia Arusha na mikoa yote ya Tanzania kupitia mawakala mbalimbali wa usambazaji wa kazi za waimbaji wa nyimbo za Injili.

Kwa mawasiliano zaidi kuhusu uzinduzi wa album hizi na jinsi ya kuzipata nakala za album hizi wasiliana na muimbaji Rose Mollel (Chipe) Kupitia:

Simu/WhatsApp: +255759 085 181, +255 658 085 181, 255 764 107 111
Instagram: @rose_chipe
Facebook: Rose Chipe
Youtube: Rose Mollel

Like Page yetu ya facebook > GOSPOMEDIA.COM instagram: @gospomedia

More in Uncategorized

To Top