Uncategorized

Albamu Mpya ya Mwimbaji Tasha Cobbs Leonard Yashika Namba Moja Kwenye Chati za BillBoard

Albamu mpya ya mwimbaji mahiri kutoka nchini marekani Tasha Cobbs iitwayo Heart, Passion, Pursuit  iliyoachiwa Agosti 25 mwaka huu ndio albamu iliyoshika namba moja kwenye chati za Billboard katika kipengele cha muziki wa Injili, na imekuwa albamu ya nane kwa jumla ya albamu zote zilinazofanya vizuri kwasasa duniani.

Tasha Cobbs ambaye mwezi mmoja uliopita alipata misukosuko ya vipingamizi na malalamiko mengi kutoka kwa mashabiki zake na wadau wa muziki wa Injili mara baada ya kutoka kwa taarifa rasmi inayohusu kumshirikisha rapa maarufu wa muziki wa secular Nick Minaji katika wimbo wake uitwao ”I’am Getting Ready” ikiwa ni moja ya nyimbo zilizo kwenye album hiyo mpya, Japo Tasha Cobbs alijitahidi kujibu vizuri juu ya kile kilichokuwa kinashutumiwa kuwa sio sawa kwa mwimbaji wa Injili kushirikiana na waimbaji wa kidunia(wanamuziki wa Secular).

“Nimemuona Nicki ambaye yupo nje ya jukwaa akiwa ana uhusiano mzuri na Mungu. Kazi yangu katika wimbo huu ilikuwa ni kuwafikia watu fulani, ” Tasha Leonard alisema. “Wasikilizaji wengine hawajawahi kumwona Mungu na sasa kupitia Nick Minaj amewafikia na kuwafunua wasikilizaji hao kwa njia yake na kwa Mungu anayempenda.”

Leonard aliongeza kuwa kwa sababu ya shuhuda mbalimbali ambazo anaendelea kupokea na kusikia kutokana na album hii anakiri atafanya tena ili kuwavuta watu wote wasioamini katika uwepo wa Mungu duniani kuwafanya kuamini na kutumika kwake vile ipasavyo.

“Ushuhuda ambao umekuja kwa sababu ya jambo hili umenisukuma kukiri kuwa nitafanya tena. Nimepokea jumbe mbalimbali kutoka kwa maelfu ya watu wakiniambia, ‘Hii ni mara ya kwanza kununua albamu ya injili. Hii ni mara ya kwanza kuwahi kumwona Mungu. Sikuamini Mungu mpaka niliposikia wimbo huu. ” Aliongeza mwimbaji Tasha Cobbs Leonard.

Kama bado hujawahi kusikia wimbo uitwao ”I’am Getting Ready” kutoka kwa Tasha Cobbs Leonard akiwa na rapa Nick Minaj, usijari Tumekusogezea tena hapa uweze kusikiliza na kupakua wimbo huu ambao ni hakika umekuwa gumzo duniani kote. Karibu ubarikiwe!!

Download Audio

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Download Audio: Luiz Feat Gudiipyne - He Reigns

Next post

Download Music Audio: Makene Feat. Bahati Kihayile - Maji ya Uzima