Connect with us

Akubali Kumuoa Mama Mwenye Watoto 10 Kutoka kwa Baba Tofauti

Jamaa-Akubali-Kumuoa-Mama-Mwenye-Watoto-10-Kutoka-kwa-Baba-Tofauti

Top Stories

Akubali Kumuoa Mama Mwenye Watoto 10 Kutoka kwa Baba Tofauti

Na Mwandishi Wetu,

Hii ni ushuhuda wa Janet, ambaye alikutana na mume wake Jackson siku ya harusi yao. Akizungumza kwenye mahojiano na Afrimax, Janet alisema mume wake ambaye alikuwa anaishi Marekani, alimjua baada ya video yake kusambaa akisimulia namna alivyoacha ukahaba na kuokoka.

Alisema video hiyo ilimfanya kujihisi kudhalilishwa baada ya kuchapishwa bila ruhusa yake lakini ilimvutia mwanamume mmoja ambaye aliguswa na ushuhuda wake. “Aliona ushuhuda wangu na aliguswa. Alihisi kwamba tunaweza kuishi pamoja milele,” alisema. Alitafuta nambari zake za simu akiwa Marekani na baada ya kuzipata alimpigia na kuanza urafiki.

Walikuwa wakizungumza kila siku na mahusiano yao yalikolea na kuwa dhabiti, alimposa kupitia simu na kisha punde si punde mipango ya harusi ilianza. Jamaa huyo hakubabaishwa na ukweli kuwa mama huyo ana watoto 10 ambao aliwazaa akiwa kahaba. Hakubabaishwa na maisha yake ya zamani, alichagua kumuoa mwanamke ambaye alikuwa anajitahidi kuishi maisha mapya. Janet alisema alikumbana na pingamizi kutoka katika kanisa lake kwa kumuona kama mwenye dhambi kubwa zaidi na hakustahili kufunga ndoa lakini alikumbatiwa na kanisa lingine ambalo liliidhinisha ndoa yake Disemba 2020.

Siku ya harusi hiyo, ndege ya bwana harusi ilitua na kukutana na mke wake kwa mara ya kwanza na kisha wawili hao walibadilishana viapo vya ndoa. Baada ya kubadilishana viapo vya ndoa, wapenzi hao walikaa pamoja kwa wiki kadhaa kabla ya mwanamume huyo kurejea Marekani na kuanza mipango ya Janet kuhamia nchini humo.

Chanzo: TUKO

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Advertisement

TRENDING

Jiunge Nasi

Jiunge na blog ya gospomedia.com ili uwe wa kwanza kupokea updates za kiinjili kila siku kupitia barua pepe yako.

Join 16,082 other subscribers

To Top