Connect with us

Aina 15 za wanawake wanaoangamiza ulimwengu wa leo

Maarifa

Aina 15 za wanawake wanaoangamiza ulimwengu wa leo

Na Flora Wingia,

Mpenzi msomaji wangu kupitia blog ya gospomedia.com kuna kipindi cha nyuma niliwahi kuandika Makala iliyobeba kichwa kinachosema Ijue nguvu iliyo ndani ya mwanamke,

Nikasema kwamba, hata kama mwanaume akiwa mtu mkuu sana katika maisha yake, lazima ajue kuwa kuna wakati alikuwa kichanga katika tumbo la mwanamke. Shetani anajua kuwa mwanamke anatawala/anamiliki uzao(tumbo la uzazi), chimbuko(chanzo, asili) na pia anatawala jiko.

Leo naomba nijikite kuelimisha aina za wanawake ambao wanaangamiza ulimwengu ama kwa kujua au kutojua kutokana na nguvu ya Ibilisi shetani iliyowazingira. Nilisema katika makala ile kwamba shetani anayo hasira kali sana dhidi ya mwanamke kutokana na nguvu kubwa iliyo ndani yake. Kama wanawake wangejua wako katika vita kali, wangeacha kubaki katika hali ya ulimbukeni na kupanga mashambulizi dhidi ya adui yao shetani.

Hebu sasa msomaji wangu tuangalie aina za wanawake wanaoangamiza ulimwengu kama zilivyochambuliwa kwenye kitabu cha ’Mwanamke Jitambue’ kilichoandikwa na mtumishi wa Mungu, Nabii B. G. Malisa wa Kanisa la Ukombozi Ministry for all Nations, lenye makao makuu jijini Mwanza na makanisa sehemu mbalimbali nchini ikiwamo hapa Jijini Dar es Salaam;

 1. Wanawake waliojiachia: Aina hii ya wanawake ni wanawake wenye aibu kidogo au hawana aibu kabisa. Wao hujihusisha kimapenzi na mwanaume yoyote aliyevaa suruali.
 2. Mbwa wa kike: Aina hii ya wanawake wanafanya kazi/wana tabia kama mbwa. Wao hujigonga kimapenzi na mwanaume yoyote aliyevaa suruali.
 3. Wanawake wa ndiyo: Hawa ni wale wanaokubali kila kitu. Hawawezi kupinga chochote hata kama wanajua kuwa wataumia mwisho wa siku, hawapingi.
 4. Wanawake wambea/ wasengenyaji: Aina hii ya wanawake ni wambea wa kumuongelea kila mtu, hata wanaume zao. Hawa wanawake husengenya hata viongozi wa dini/watumishi wa Mungu (wachungaji, mapadri, mashekhe).
 5. Wanawake wachawi: Ulimwengu wa kichawi unamilikiwa na wanawake. Kama Mungu angefungua macho yako kuona makundi ya wachawi, ungegundua kuwa wengi wao ni wanawake.
 6. Wanawake waongo: Hawa ni mabingwa katika kusema uongo. Huwa hawasemi ukweli. Wanaweza kukwambia mvua inanyesha wakati hainyeshi.
 7. Wanawake wenye ufahamu mdogo: Wanawake wa aina hii, ufahamu wao ni mdogo. Hawawezi kupanga kitu chochote cha maana. Hawa hawamaanishi kufanya chochote katika maisha yao.
 8. Wanawake wanaojichanganya kwenye ngono: Hawa ni wanawake wanaofanya kila aina ya uovu wa ngono, mfano wanachanganya uzinzi, uasherati, usagaji, wanazini na wanyama, miti na kadhalika. Wamechanganyikiwa.
 9. Wanawake dume (Wenye roho za kiume): Hawa wana tabia kama wanaume. Wao wanawatawala wanaume zao. Wanawaamuru waume zao kana kwamba wao ni vichwa. Wanawake wa aina hii huishia kuwafukuza/kuwafanya wanaume wazikimbie ndoa zao.
 10. Wanawake wenye hisia zilizopitiliza au wastaarabu kuliko kawaida: Hawa siku zote hawawezi kuwa halisi. Siku zote huonyesha hisia zao zote katika maongezi yao au katika maisha yao ya kila siku. Ni wastaarabu kuliko kawaida. Wao hupenda kuhudhuria makanisa ambayo mchungaji anaweza kuwasiliana na simu akiwa tayari amesimama madhabahuni. Hawapendi kuambiwa ukweli kuhusu maisha yao. Hawapendi kuabudu kwenye makanisa yanayofundisha ukweli, yenye maombi makali ya kutoka jasho, maana hawapendi kuchafuka au kutoka jasho wakiwa katika nyumba ya ibada.
 1. Wanawake wenye majivuno/ufahari/ukuu: Ni wanawake ambao hawathamini watu wengine. Wao hujiona kuwa ni viumbe walioumbwa vizuri na Mungu kuliko wanadamu wengine.Wana majivuno sana.
 2. Wanawake wanaoshinda kando ya barabara: Hawa ni wanawake wanaojirahisisha sana. Wanajifanya ni wema sana kiasi cha kuzini na kila mwanaume anayewataka. Na kama wanaume wangeacha tabia ya kuwataka, hawa wanawake wangetoka barabarani.
 3. Wanawake wanaochukuliwa na kila aina ya upepo: Hawa wakiambiwa lia, wanalia, wakiambiwa kucheka nao hucheka. Wakisikia mtu anasema; sasa wanawake wanatakiwa kuvaa suruali za kubana, ndio fasheni, wengi watafungua kabati na kuvaa hizo suruali. Hawana msimamo binafsi.
 4. Wanawake vigeugeu: leo wanacheka, wana furaha lakini kesho wamekwisha kubadilika. Ni wanawake waliojaa huzuni na hasira kila mara.
 5. Aina zingine ni wanawake wavivu/wazembe, wasio na maana/wapumbavu: Wanavaa vizuri lakini ni wapumbavu-mavazi ya aibu, wanawake sugu, wachonganishi, hawa kila wanapokwenda huwachanganya watu hata maofisini na wanaongea vitu tofauti kwa watu na kuwagonganisha, wezi wa waume za watu hawa wana upako tofauti sana wa kishetani wa kuiba waume za watu. Hawa ni wanawake wanaoangamiza ulimwengu.

Niishie hapa, naamini umejifunza kitu hapo. Wiki ijayo: Jiko ni silaha kubwa ya mwanamke dhidi ya maadui! Usikose.

Je, una jambo la kimaisha linakutatiza? Lete tujadiliane. Ukiwa tayari kuwa huru kuwasiliana nami kwa ujumbe mfupi kupitia simu ya ofisi namba 0715268581 (usipige).

Like us on facebook >> Gospo Media Follow us on instagram >> @gospomedia

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Maarifa

To Top