Connect with us

Aina 14 za Hasira Walizonazo Wanawake

Aina 14 za Hasira Walizonazo Wanawake

Dondoo

Aina 14 za Hasira Walizonazo Wanawake

1. Kuna mwanamke ambaye akikasirika, huishia kulia tuu!

2. Mwanamke mwingine akichukia, anaongea sana muda wote mpaka kero kwa wanaomzunguka.

3. Mwanamke mwingine akikasirika, ananuna, haongei! Mtapishana tu kimya kimya. Mawasiliano kibubu-bubu. mashavu yamevimba kwa hasira.

4. Mwingine akishikwa na hasira, period ya ghafla ghafla inafuata!

5. Wako wanawake ambao, akichukia, Atakachokishika usipokimbia anakutandika na anaweza kukuchoma na kisu, majuto baadaye!

6. Mwanamke mwingine akikasirika, hasira zake zinaishia kwenye kuvunja-vunja vyombo. Au saa nyingine kugombeza-gombeza wafanyakazi na watoto! Dizaini hii, huwa ni wale waliokosa kukidhiwa haja za kihisia/ndoa na waume zao!

7. Mwanamke mwingine akikasirika, Mtajuana kitandani panapo usiku.

8. Kuna wanawake wengine wakitibuliwa, hukimbilia kufunga mabegi na kuondoka!

9. Wapo wanawake ambao wakikasirika, Wanagoma kupika!

10. Wanawake Wengine wakichukia, Wanaamua kwenda kulala kimya kimya!!

11. Wanawake wengine wakikasirika, tumbo linakata, na pengine mpaka wanaharisha!

13. Wako ambao wakishikwa na hasira, huingia kwenye maombi na kuugua kusikoweza kutamkwa. Uchungu ukiisha, wananawa uso na kwenda sokoni.

14. Yuko ambaye akishikwa na hasira, hucheka sana…. Hutajua kama amekasirika! Aina hii ya hasira ni hatari sana, maana inaweza kukudhuru kiurahisi.

Mwanamke Tumia Mistari hii ikusaidie:

Epuka hasira na uache ghadhabu, usihangaike: itakuongoza tu kutenda uovu. Zaburi 37:8

Mtu mwenye hasira huchochea ugomvi, naye mtu mwenye hasira ya haraka hutenda dhambi nyingi. Mithali 29:22

hasira ya mwanadamu haitendi haki ya Mungu. Yakobo 1:20

WANAUME:

Ninyi waume, wapendeni wake zenu, wala msiwe na uchungu dhidi yao. Wakolosai 3:19

WANANDOA:

Mkikasirika, msitende dhambi, wala jua lisichwe mkiwa bado mmekasirika, Waefeso 4:26

Vumilianeni na kusameheana mtu akiwa na lalamiko lolote dhidi ya mwenzake. Sameheaneni kama vile Bwana alivyowasamehe ninyi. Wakolosai 3:13

 

1 Comment

1 Comment

  1. Bm

    September 9, 2021 at 5:07 pm

    Ok

Leave a Reply

Your email address will not be published.

To Top