Uncategorized

AFYA: USISUMBUKE KUTAFUTA DAWA YA MBA,TIBA YAKE ASILIA HII HAPA

MBA (Yeast/Hamira) ni jamii ya fangasi ambao hushambulia mwili/ngozi. Mba ni jamii hiyo. Maeneo yenye mabaka yanayoletwa na fangasi wa aina hii hubadilika rangi yake na kuwa na rangi hafifu au inayoonekana zaidi (kama ni mtu mwenye rangi ya maji ya kunde basi ngozi iliyoathiriwa hubadilika na kuwa nyeupe au nyeusi sana.Hali hii hutokana na uwezo wa fangasi wa aina hii kusimamisha shughuli za uzalishaji wa homoni na kemikali inayoipa ngozi rangi yake. Hii husababisha upungufu wa kemikali na hivyo mabadiliko ya rangi ya ngozi.
NANI YUPO KWENYE HATARI YA KUPATA TATIZO HILI?
watoto, watu wenye uzito mkubwa, wagonjwa wa kisukari, watu wenye upungufu wa madini ya chuma na zinki, wajawazito , wanaofanya kazi katika mazingira yenye unyevu , watu wenye kinga hafifu ya mwili n.k
TIBA
Maradhi haya huweza kutibika kirahisi, ila mara nyingi hurudia kushambulia ngozi hasa eneo ambalo liliwahi kushambuliwa kabla. Matibabu ya maradhi haya huhusisha dawa za kupaka zinazoua vimelea hivi vya fangasi.
Dawa za kuua vimelea vya fangasi za kunywa pia hutolewa kwa ajili ya kutibu aina hii ya fangasi lakini hushauriwa zitolewe tu kama dawa za kupaka zimeshindwa kuua vimelea hivi vya fangasi.
TIBA YA ASILI
vitu vya asili vilivyothibitika kua na uwezo wa kupambana na fangasi hawa ni pamoja na maziwa ya mgando , mafuta ya Nazi, kitunguu swaumu na tangawizi . Baada ya kupata tiba hali ya sehemu ya ngozi iliyoathiriwa na vimelea vya fangasi kurudisha rangi ya kawaida ya ngozi kama sehemu nyingine ambazo hazikua na madhara huchukua muda mrefu kidogo kutegemea na mtu na mtu ingawa kama eneo husika lilikua na uvimbe basi uvimbe hupotea haraka.
Imeletwa kwenu na Jukwaa la Afya, 0764265678

Advertisements
Previous post

MIKE SAMA KUACHIA NGOMA MPYA

Next post

VIDEO: MCHUNGAJI GEORDAVIE AELEZEA JINSI ALIVYOMTABIRI MAGUFULI KUWA RAIS.