Audio

Audio: AD Music Feat. Happy – Imara

Baada ya kufanya vizuri mwaka 2017 kupitia video iitwayo Kimbilio kwa mara nyingine tena katika mwaka 2018 kundi la waimbaji wa nyimbo za Injili linalofahamika kwa jina la AD Music lililopo jijini Arusha wanautambulisha kwako wimbo wao mpya uitwao IMARA safari hii wakiwa wamemshirikisha mwanadada Happy. Muziki huu umetayaarishwa ndani ya studio za DM Records chini ya mikono ya prodyuza Deon Beats.

Kwa mujibu wa kiongozi wa kundi la AD Music, Agust Luck alisema:-

”Katika wimbo huu wa Imara tumezungumzia uimara ambao unapatikana ndani ya kumtumikia Mungu na kutojiwekea hofu ndani maana mtetezi Yesu bado yu hai. Pia inaonyesha kimbilio letu ni Yesu tu na ndio msaada wetu hakuna cha kuogopa ukiwa naye na kusimama imara bila kutetereka. Mithali 18:10.  Jina la BWANA ni ngome imara; Mwenye haki huikimbilia, akawa salama.” – Alieleza

Kundi la AD Music linaundwa na vijana watatu ambao ni Agustino Lucas(Agust luck), David Jackson na Parlicio Felicidades na tulipopata nafasi ya kuzungumza na kiongozi wa kundi hilo kuhusiana na mwelekeo wa kundi lao na huduma yao kwa ujumla alisema kuwa kwasasa wamejipanga kuachia kazi nzuri zaidi ambazo wanaamii zitakuwa ni zenye kuwabariki watu wengi zaidi hasa katika kipindi hiki ambacho watu wamekuwa katika shida mbalimbali lengo ni kuihubiri Injili ziguse nafsi na mioyo yao ili waizidi kumuanini Mungu na kuacha imani potofu za shetani.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza wimbo huu ambao nina hakika utakwenda kukuimarisha kukupa nguvu mpya ya mafanikio.. Barikiwa.

 

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na uongozi wa kundi la AD Music kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 759 669 805, +255 676 762 575
Facebook: Agust luck | David Jackson | AD Music
Instagram: @agustluck | @ad_music

Like us on facebook >> GOSPO MEDIA  Follow us on instagram >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Video | Audio: Goodluck Gozbert - Hauwezi Kushindana

Next post

Video | Audio: Shadrack Robert - Wimbo