Connect with us

Audio: Ambwene Mwasongwe – Jiwe

Audio

Audio: Ambwene Mwasongwe – Jiwe

Kutoka kwa mwimbaji mkongwe katika kiwanda cha muziki wa nyimbo za Injili Tanzania maarufu kwa jina la Ambwene Mwasongwe ambaye hivi karibuni alifanikiwa kufunga pingu za maisha na sasa ameachia wimbo wake mpya uitwao Jiwe.

Jiwe ni wimbo unaomuelezea Mungu kwa lugha ya picha ambapo katika wimbo huu mtumishi wa Mungu Ambwene Mwasongwe ametumia taswira ya Jiwe kama moja ya sifa ya Mungu katika kutetea na kulinda maisha yetu sisi watoto wake. Yeye ni Jiwe, Yeye ni jabali, Yeye ni simba huunguruma, Yeye ni Mungu mkuu, Yeye ni mwalimu mkuu, Yeye kuhani mkuu.

Hii ni moja kati ya kazi bora kabisa kwa mwaka 2018 ambazo hutaacha kuzisikiliza mara kwa mara na hakika Mungu atajidhihirisha katika maisha yako, Kwakuwa yeye ni Jiwe, Yeye ni Jabali, Yesu.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kupakua wimbo huu hapa, Barikiwa.

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Ambwene Mwasongwe kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 767 619 931
Facebook: Ambwene Mwasongwe
Instagram: @ambwenemwasongwe_official
Youtube: Ambwene Mwasongwe

Like us on facebook >> Gospo Media Follow us on instagram >> @gospomedia

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Audio

To Top