Video | Audio: Borne Kingz - Fire - Gospo Media
Connect with us

Video | Audio: Borne Kingz – Fire

Audio

Video | Audio: Borne Kingz – Fire

Baada ya kimya cha takribani mwaka mmoja toka walipoachia wimbo wao uitwao “Hello” kundi la waimbaji wa nyimbo za Injili kwa mtindo wa HipHop linalofahamika kama Borne Kingz, Kwa mara ya kwanza katika mwaka 2018 wamekuja kivingine kwa kuachia video ya wimbo wao mpya iliyobeba jina la “Fire”. Video ikiwa imeongozwa na director Yotham Liyhoba na kuhaririwa na Lamasias, Muziki huu umetayaarishwa na mikono ya prodyuza Innocent Mujwahuki na kurekodiwa ndani ya studio za Push Up Records.

“Fire” ni wimbo uliojaa sifa na wenye kumtukuza Mungu kwa matendo yake makuu katika maisha yetu, Bwana Yesu aendelee kushusha moto wa Baraka juu ya maisha yako kama unaamini katika yeye, endelea kusifu na kumtukuza Mungu siku zote na moto wa Baraka uzidi kushuka juu yako.

Borne kingz ni kundi linalowaunganisha vijana watatu ambao ni Ellyjoh, Lamasias pamoja na Elandre. Kundi hili liliundwa tangu mwaka 2011 kwa nia njema ya kumtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji. Maana halisi au kirefu cha BORNE KINGZ ni “Bearing the Mark of the King” ikimaanisha “Wabeba Chapa ya Kifalme”.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kutazama video hii na kupakua wimbo huu ambao nina imani utaufurahia na kukubariki, Ameen.

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na kundi uongozi wa kundi la Borne Kingz kupitia:

Simu/Whatapp: +255 717 057 457
Facebook page: Borne Kingz
Instagram: @bornekingz @pushuprecords @mujwahukii @iamelandre @lamasias @ellyjoh255 @emmanuelgripa
Email: bornekingztz@gmail.com

Like us on facebook >> Gospo Media Follow us on instagram >> @gospomedia

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Audio

To Top