Video | Audio: Abeid Makarabo - Afya ya Roho - Gospo Media
Connect with us

Video | Audio: Abeid Makarabo – Afya ya Roho

Audio

Video | Audio: Abeid Makarabo – Afya ya Roho

Abeid Makarabo ni mwimbaji mpya katika kiwanda cha muziki wa Injili aliyeanza kunekana kufanya vizuri baada ya kuachia wimbo wake mzuri na wenye kugusa uitwao Afya ya Roho na sasa ameshaachia video ya wimbo huo ikiwa imeongozwa na kampuni ya Creato Pro Films, Muziki ukiwa umetayaarishwa na kurekodiwa ndani ya studio za Chosen Records International zilizopo jijini Dar es salaam.

Afya ya Roho ni wimbo uliobeba ujumbe unaotukumbusha juu matunda tisa ya roho ambayo yanampa mkristo afya na kinga bora kiroho na endapo mtu yeyote atakosa chakula hicho kuna hatari kubwa ya kushambuliwa na majaribu na kushindwa kustahimili changamoto za kiroho na kimwili, Hivyo kupitia wimbo huu tunakumbushwa na kusisitizwa kuwa na mazoea ya kuzilisha roho zetu chakula bora cha kiroho ili tuweze kuwa na afya na kinga imara ili tuweze kupigana vita na kushinda majaribu.  Upendo, Furaha, Amani, Uvumilivu, Utu Wema, Fadhili, Uaminifu, Upole na Kiasi Haya ndio matunda tisa aliyotufundisha Baba.

Abeid Makarabo ni kijana ambaye ameamua kuyatoa maisha yake katika kumtumikia Mungu kama shukrani ya kumnusuru na mauti baada ya kuugua kwa muda mrefu maradhi yaliyopelekea kupoteza uwezo wake wa kutembea (kupooza).

Licha ya kuwa katika hali hii ya ugonjwa uliomtesa ka muda mrefu, Abeid hakumuacha Mungu, aliendelea kumtumikia Bwana akiwa kwenye kiti maalumu cha magurudumu (wheelchair ), Ushuhuda wa Abeid juu kile kilichomsibu una mambo mengi ambayo hugusa mioyo ya watu wengi, na ndio sababu ya kuandika na kuimba wimbo huu Afya ya Roho ambao nina hakika hata wewe utakugusa kwa namna ya pekee.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha sasa kuitazama video hii njema na kupakua wimbo huu ambao nina imani kuwa utakubariki na kukuinua katika viwango vya juu kabisa kiroho, Barikiwa.

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Abeid Makarabo kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 763 044 880
Facebook: Abeid Makarabo
Instagram: @abeid_tz
Youtube: Abeid Makarabo

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Audio

To Top