Video | Audio: Mwamini Muyero-Wema wa Mungu - Gospo Media
Connect with us

Video | Audio: Mwamini Muyero-Wema wa Mungu

Audio

Video | Audio: Mwamini Muyero-Wema wa Mungu

Moja kati ya waimbaji wanaoendelea kufanya vizuri mwaka 2018 katika kiwanda cha muziki Tanzania ni pamoja na mwimbaji Mwamini Muyero ambaye kwasasa anatamba na video yake iitwayo “Yesu Usifiwe” aliyoiachia mwezi wa tatu na kwa mara nyingine tena ameachia tena video yake mpya iitwayo “Wema wa Mungu” ikiwa imeongozwa na director Mbangwa Hassan na muziki ukiwa umetayaarishwa na kurekodiwa ndani ya studio za Soft Records chini ya mikono ya prodyuza Pitshou Mesha.

“Karibu ubarikiwe na wimbo wangu huu mpya, Napenda kukumbusha tu kuwa Wema wa Mungu katika maisha yetu umetuzunguka. Ukiomba na kuamini hakuna jambo lolote baya litakaloweza kutuvuruga simama imara ukimtumainia Bwana ambaye aliushinda ulimwengu kwa damu yake ya pekee iliyomwagika msalabani, Wema wa Mungu ukuzunguke leo na hata milele, Barikiwa.” – alisema Mwamini.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kutazama video hii njema nikiamini utabarikiwa na kuinuliwa kwa ujumbe uliojaa matumaini na nguvu ya imani kwa ajili yako, Wema wa Mungu uzidi kutawala maishani mwako, Amen.

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Mwamini Muyero kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 769 698 909
Facebook: Mwamini Muyero
Instagram: @officialmwamini
YouTube: Mwamini Muyero

Like us on facebook >> Gospo Media Follow us on instagram >> @gospomedia

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Audio

To Top