Connect with us

Mfahamu Liberatus Katabazi na safari yake huduma ya muziki wa Injili

Habari

Mfahamu Liberatus Katabazi na safari yake huduma ya muziki wa Injili

Liberatus Katabazi ni mwimbaji wa nyimbo za injili kwa zaidi ya miaka  kumi sasa katika huduma akiwa ni mzaliwa katika wilaya ya Karagwe mkoa wa Kagera nchini Tanzania.

Katabazi ameishi na kusoma katika shule na vyuo mbalimbali ikiwemo Sengerema Sekondari, Ukiriguru  na Sokoine chuo kikuu cha kilimo vyote vikiwa nchini Tanzania. Kwa sasa Liberatus katabazi anasoma shahada yake ya Pili (Masters) katika sayansi ya Wanyama katika Chuo kikuu Sydney kilichopo nchini Australia.

Katabazi amefanya huduma mbalimbali katika vikundi  kama CASFETA, TAFES, UPSF, na ushirika wa kikristo wa wanafunzi katika maeneo yote alikopita na huduma yake kubwa imekuwa ni uimbaji na Kufundisha waimbaji wa sifa na kwaya makanisani na vyuoni, Kwaya ambazo amewahi kufundisha ni pamoja na UPSF kwaya ya SUA Morogoro.

Safari ya Muziki

Liberatus Katabazi ameanza huduma ya uimbaji akiwa angali mtoto akiimba kwaya ya watoto kanisani, shuleni katika kwaya na mashindano ya michezo kwa shule mbalimbali. Katabazi amekuwa akitunga na kufundisha nyimbo kwa vikundi mbalimbali.

Kwa mara ya kwanza Katabazi alirekodi album yake ya kwanza katika mfumo wa Audio mwaka 2011 iliyokwenda kwa jina la Ndivyo Tulivyo ikiwa na mkusanyiko wa nyimbo tisa, Nyimbo hizo ni pamoja na Ndivyo Tulivyo, Nakuabudu, Jina lako, Mtakatifu, Watu wa Mungu n.k.

Baada ya Kimya cha mda mrefu Liberatus kwasasa ameamua kuachia video ya wimbo wake wa kwanza uitwao Ndivyo Tulivyo ikiwa ni wimbo unaobeba jina la album na huu utakuwa ni mfululizo wa video zingine zitakazofuatia baada ya video hii aliyoiachia mwezi wa sita 2018.

Liberatus anazo nyimbo nyingine nyingi ambazo kwasasa zipo katika maandalizi na Mungu atakapompa kibali ataweza kuziachia. Ameiambia gospomedia.com kuwa DVD ya album yake itakuwa tayari kufikia mwisho wa mwezi wa saba (July) mwaka huu, Lakini pia anatarajia kuachia album yake mpya ifikapo mwisho wa mwaka huu.

Nyimbo zote audio za mwimbaji Liberatus Katabazi zinapatikana katika mtandao kupitia ukurasa wake wa YouTube kwa jina la LIBERATUS KATABAZI/BALOZI K- GOSPEL NEWS na site nyingine kama itune

Malengo yake: Kufanya huduma kwa namna ya tofauti katika muziki na kuendelea kuipeleka injili kwa njia ya muziki wake. Anawakaribisha watu wote kutembelea kurasa zake YouTube, Facebook, Twitter, Instagram na kufuatilia habari na matukio yote yanayomhusu.

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Liberatus Katabazi kupitia:
Simu/WhatsApp: +61 416 376 192(Australia), +255 753 748 908(Tanzania), +255 769 601 266(Tanzania)
Facebook: Liberatus Katabazi
Instagram: @libekata
Twittter: @liberatusV Email: libekata@gmail.com
Youtube: BALOZI K – GOSPEL NEWS

Like us on facebook >> Gospo Media Follow us on instagram >> @gospomedia

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Habari

To Top