Video | Audio: David Wonder - Msalaba - Gospo Media
Connect with us

Video | Audio: David Wonder – Msalaba

Audio

Video | Audio: David Wonder – Msalaba

David Wonder ni moja kati ya waimbaji wapya wanaoendelea kufanya vizuri zaidi katika huduma ya muziki wa Injili nchini Kenya na kwa mara nyingine tena katika mwaka 2018 ameachia video ya wimbo wake mzuri uitwao Msalaba, Video hii imeongozwa na director Rahim, Na Muziki ukiwa umetayaarishwa na kurekodiwa ndani ya studio za EMB Records.

Msalaba ni wimbo unaotukumbusha juu ya wokovu wetu ambao ulipatikana kupitia mateso na kifo cha Bwana wetu Yesu Kristo, Kupitia msalaba wake alimaliza dhambi zetu, mateso na shida zetu zote. 1 Petro 2:24
Yeye mwenyewe alizibeba dhambi zetu katika mwili wake juu ya msalaba, tupate kufa kuhusu dhambi, na kuishi kwa ajili ya uadilifu. Kwa majeraha yake, nyinyi mmeponywa.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kutazama video hii, ni imani yangu kuwa utabarikiwa na kuguswa na wimbo huu, Bwana Yesu Asifiwe!

Download Audio

Social Media
Facebook: David Wonder EMB
Instagram: @davidwonderemb
Twittter: @davidwonderemb

Like us on facebook >> Gospo Media  Follow us on instagram >> @gospomedia

More in Audio

To Top