Habari

Kongamano la wanawake waombolezao kitaifa kuanza Julai 26, 2018

Na Mwandishi wetu,

Mara baada ya kupata mafanikio makubwa mwaka 2017, Kwa mara nyingine tena, Kongamano kubwa la wanawake waombolezao kitaifa linatarajiwa kuanza Julai 26 hadi tarehe 28, 2018, Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mh. Mama Janeth Magufuli.

Akiongea na gospomedia.com Mwenyekiti wa kongamano hilo mchungaji Debora Malassy wa kanisa la Tanzania Fellowship of Churches amesema kuwa, Nia na madhumuni ya kongamano hilo ni kuliombea Taifa letu la Tanzania liendelee kuwa na amani na utulivu pamoja na kuombea ndoa, familia na biashara zetu. Hivyo Kamati ya maandalizi ya kongamano la Wanawake Waombolezao Kitaifa inapenda kuwakaribisha wanawake wote bila kujali dini, dhehebu wala itikadi zao.

Kongamano hili ambalo hufanyika mara moja tu kwa mwaka litakuwa ni la aina yake  likiwakusanya wanawake wawakilishi kutoka mikoa yote ya Tanzania pamoja na Zanzibar na wake wa viongozi wa Tanzania pamoja na wake wa mabalozi wa nchi mbalimbali walioko nchini Tanzania.

Kongamano la Wanawake waombolezao Kitaifa linatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Millenium Towers ghorofa ya kwanza Mtana hall, kuanzia siku ya Alhamisi ya tarehe 26.7.2018 saa 8 mchana hadi 12:30 jioni, Na tarehe 27 Ijumaa na tarehe 28 Jumamosi kongamano litaanza saa 3 asubuhi hadi jioni. Aliongeza

Mbali na shughuli hiyo pia kutakuwa na sare ya vitenge vitakayouzwa kwa shilingi 25,000/= tu.  Hakuna kiingilio, Na watu wote mnakaribishwa.

Kwa mawasiliano zaidi na maelekezo wasiliana na Mwenyekiti wa kongamano Mchungaji Deborah Malassy kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 754 515 215
Facebook: tfccellchurches
Instagram: @tfccellchurches

Like us on facebook >> Gospo Media Follow us on instagram >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Video | Audio: Theofrida Gervas - Kama Siyo Wewe

Next post

Video | Audio: Havoc Musiq - Atatenda