AudioVideo

Video | Audio: Dona JR Feat. Miriam Jackson & Prophet Bashando – Do it Now

Moja ya Rapa mahiri wanaoendelea kufanya vizuri katika kiwanda cha muziki wa Injili Tanzania ni pamoja na Dona JR ambaye ameonekana kuendelea kuachia nyimbo zenye mguso na kutoa matumaini kwa watu wengi hii ni baada ya kuachia wimbo wake uitwao “Narudi” mwezi Februari 2018 akiwa amemshirikisha mwanadada Rebecca na sasa  ameachia video ya wimbo wake mpya kabisa uitwao DO IT NOW akiwa amemshirikisha mwanadada Miriam Jackson pamoja na rapa mahiri anayefahamika kama Prophet Bashando.

Video hii imeongozwa na director HOBO kutoka studio za HB Filmz na Muziki ukiwa umetayarishwa na kurekodiwa ndani ya studio za Enzi Records chini ya mikono ya prodyuza Amzy.

“DO IT NOW ni wimbo ambao unasisitiza watu hasa vijana kutokata tamaa na kufanya vitu bila kupoteza muda (without delaying) Kama neno la Mungu linavyotuambia kuwa WAKATI WA WOKOVU NI SASA na kulingana na asili ya maisha yetu kwa sasa umri wa kuishi umepungua hivyo tunatakiwa tufanye kazi ya Bwana kama mwisho wa dunia ni kesho (yaani wakati ambao Masihi anakuja kulichukua kanisa) kwa hiyo ukipata nafasi ya kufanya kitu kwa ajili ya Mungu fanya hadi kile kitu unachokifanya kijue kwamba wewe ndo umeagizwa na Mungu ukifanye (MAKE THE PERFECT FOR EVERY OPPORTUNITY) Fanya sasa #DOITNOW. ” – Alisema Dona.

1 Petro 4:10
Kila mmoja anapaswa kutumia kipaji alichojaliwa na Mungu kwa faida ya wengine kama wakili mwema wa zawadi mbalimbali za Mungu. Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza wimbo huu nikiamini kuwa utakwenda kubadilisha maisha yako kuanzia sasa. DO IT NOW !!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na rapa Dona JR kupitia:-
Simu/WhatsApp: +255 746 083 735, +255 713 02 44 55
Facebook: Donanciano Van Joseph
Instagram: @255dona
Twitter: @255dona
Youtube: DONA Jesus Rapper

Like us on facebook >> Gospo Media Follow us on instagram >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Audio: Paul Payne837 - Nakupeza(I've found you)

Next post

Baada ya kuokoka, je ni sahihi kibiblia kushughulika na laana au urithi wa mababu?