Habari

Waziri wa Afya atuma ujumbe mzito kwa wanamuziki wa Injili

Na Mwandishi wetu, Arusha.

Naibu Waziri wa Afya Dr. Faustine Ndungulile amewataka wanamuziki wa Injili kuimba nyimbo zinazoweza kuihamasisha jamii kushiriki katika masuala mbalimbali ikiwamo uchangiaji wa damu salama.

Akizungumza wakati wa Tamasha la Tamani Festival lililoandaliwa na Mtandao wa Wasanii wa Tasnia ya Injili (Tagoane) Dk. Ndungulile alisema yapo mambo mengi yanayohitaji ushiriki wa wasanii katika kukabiliana nayo.

“Yapo matukio yanawategemea wasanii mshiriki, imbeni nyimbo zinazoihamasisha jamii ipime magonjwa, iache uovu maana matukio ya kikatili nayo ni mengi,” alisema.

Dr. Ndungulile ambaye ni muasisi wa uchangiaji wa damu nchini alisema uhai wa mama na mtoto pia unategemea uhakika wa damu salama.

Dr. Ndungulile (kushoto) na Dr. Maimu (kulia) wakiwa ndani ya chumba cha uchangiaji wa damu.

Pia alikubali ombi la kuwa mlezi wa Tagoane akiahidi kushirikiana na wanamuziki kuhamasisha jamii kupima afya zao hasa wanaume ambao wengi hawashiriki.

Awali Rais wa Tagoane Dr. Godwin Maimu alisema taasisi hiyo imeamua kufanya tamasha la asante mama ili kuenzi mchango wa mwanamke katika jamii.

Wanachama wa TAGOANE wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu waziri.

Pamoja na mambo mengine Tagoane walishiriki kufanya usafi katika hospitali ya Mount Meru na kuhamasisha uchangiaji wa damu salama.

Like us on facebook >> Gospo Media Follow us on instagram >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Video | Audio: Joel Lwaga - Yote Mema

Next post

Audio: Profnificent - Jesu Kristi