AudioVideo

Video | Audio: Gaudence Paul – Nangojea

Gaudence Paul ni mwimbaji mpya katika huduma ya muziki wa Injili nchini Tanzania akitokea jijini Arusha na sasa ameachia video ya wimbo wake mpya uitwao Nangojea, Video hii imeongozwa na director Einxer na muziki ukiwa umetayaarishwa na kurekodiwa ndani ya studio za Apex Music chini ya mikono ya prodyuza Masai na Mr. Apex.

“NANGOJEA ni wimbo uliobeba ujumbe wenye lengo kubwa la kumtia moyo mtu yule anayepitia maisha yenye upungufu wa kitu fulani katika maisha yake, Yawekezakana kuna mtu wakati huu uchumi wake umeyumba, amefukuzwa kazi, ndoa yake haina amani, anatamani kupata mtoto, maradhi yanamsumbua na mapito mengine magumu kama hayo. Hivyo huu ni wimbo unaotukumbusha na kutufundisha kuwa na subira kwa maana kusudi la Mungu ni kumbariki kila mmoja katika majira sahihi. Barikiwa!” – alisema mwimbaji Gaudence Paul.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kutazama video hii na hakika utabarikiwa kila wakati utakapokuwa unasikiliza wimbo huu, Bwana Yesu asifiwe!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Gaudence Paul kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 759503771
Facebook: Gaudence Paul
Instagram: @gau.paul.laizer
Youtube: Gaudence Paul

Like us on facebook >> Gospo Media Follow us on instagram >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Audio: Elvis Goodluck – My God Big

Next post

Video | Audio: Hellen sogia - Nina sababu