HabariMatukio

Ibada ya “IN RYTHM” kufanyika 8 July 2018 Jijini Dar es salaam

Huduma ya Rhythms For Christ Ministry (R4C) wameandaa Ibada ya Ibada ya Sifa na kuabudu inayoitwa “IN RYTHM”. Ibada hii itafanyika siku ya jumapili ya tarehe 8 mwezi wa 7, 2018 katika kanisa la Pentecoste, Tabata Kisiwani kwa Pastor John Shusho kuanzia saa nane kamili na kuendelea.

Katika Ibada hii watahudumu watumishi mbalimbali kama vile Angel Benard, Kennedy Gerald, Elias Solomon, Elshadai Choir, Holyland Team, The Doxas na Pastor Deo Mbona.

Akizungumza na gospomedia.com mmoja wa wabeba maono wa huduma hii ya Rhythms for Christ Ministry (R4C) mtumishi Kennedy Gerald alisema:

“Tutakuwa na wakati mzuri sana wa Kumsifu na kumwabudu Mungu aliyehai na Tumejipanga kufanya ibada hizi kila baada ya miezi miwili, Kwa utukufu wa Mungu hivyo nawakumbusha na kuwasisitiza wakazi wote wa jiji la Dar es salaam na mikoa yote ya jirani kufika kwenye Ibada hii Takatifu ambayo itakwenda kubadilisha maisha ya watu wengi kupitia nguvu na uwezo wa roho mtakatifu.”

Kwa mawasiliano zaidi na wewe ambaye unahitaji kufika siku ya kesho katika ibada hii Takatifu “IN RYTHM” unaweza kuwasiliana na moja kati ya watumishi hawa kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 769 823 566

Like us on facebook >> Gospo Media Follow us on instagram >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Audio: Paul Payne837 - Nakupeza(I've found you)

Next post

Video | Audio: Dona JR Feat. Miriam Jackson & Prophet Bashando – Do it Now