Video | Audio: Janet Otieno - Asante - Gospo Media
Connect with us

Video | Audio: Janet Otieno – Asante

Audio

Video | Audio: Janet Otieno – Asante

Baada ya kufanya vizuri kupitia video ya wimbo wake uitwao “Narudi” ikiwa ni wimbo wake wa kwanza kuachia kwa mwaka 2018 mwimbaji mahiri Janet Otieno kwa mara nyingine tena ameachia video ya wimbo wake mpya uitwao “Asante”, Video hii imeongozwa na director Trey Juelz na muziki ukiwa umetayaarishwa na prodyuza Tim kutoka studio za Tim Still Alive Records.

“Madhaifu yangu, mapungufu yangu, kiburi changu umenipendea nini Baba. Ubaya wangu, shida zangu, umaskini wangu, Umenipendea nini Baba. Sina cha kujivunia, sifai mbele zako Umeamua kunipenda, niseme nini Baba yangu, Asante, asante Baba, Asante” – Janet Otieno

Hakika hii ni moja kati nyimbo nyingine nzuri na bora kabisa alizowahi kuachia Janet Otieno ikiwa imebeba ujumbe wa kumshukuru Mungu na kutukumbusha juu ya upendo mkuu wa Bwana wetu Yesu Kristo kwa ajili yetu.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kutazama video hii na kupakua wimbo huu ambao ni imani yangu utakubariki na kukuinua siku zote. Barikiwa!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na muimbaji Janet Otieno kupitia:
WhatsApp: +254 720 778494 Facebook: Janet Otieno
Instagram: @janetotienoKe
Youtube: Janet Otieno
Email: jannettn@gmail.com
Website: www.janetotieno.co.ke

Like us on facebook >> Gospo Media  Follow us on instagram >> @gospomedia

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Audio

To Top