Habari

Tagoane waitikisa Arusha kwa maandamano ya amani, kuchangia damu.

Na mwandishi wetu, Arusha

Mji waArusha leo ulizizima baada ya wadau wa Mtandao wa Wasanii wa Injili Tanzania Kwa kiingereza Tanzania Gospel Artists Network – kufanya maandamano ya amani kuhamasisha jamii kuchangia damu ili kuokoa uhai wa mama na mtoto.

Wanatagoane wakijiandaa na maandamano kuanzia Hospitali ya Mount Meru hadi uwanja wa Shekh Amria Abeid Karume baada ya kufanya usafi hospitalini hapo.

Tagoane walifanya maandamano hayo wakiongozwa na Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kiruthel Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Arusha Mashariki, Dk Solomoni Masangwa baada ya kufanya usafi na kutoa zawadi katika Hospitali ya Mount Meru kupitia tamasha la Asante mama linaloitwa TAMANI Festival.

Akizungumza kwenye maadhimisho hayo, Rais wa Tagoane Dk Godwin Maimu alisema wameamua kufanya maadhimisho hayo ili kutambua mchango wa mama katika malezi ya familia, jamii na taifa.

“Tumeanza tamasha hili leo kwa kufanya usafi, kutoa zawadi hospitalini na kufanya maandamano ili tuitumie jamii yetu ujumbe kwamba mama ni wa thamani,” alisema.

Shughuli zote za uchagiaji wa damu zinaendelea kufanywa katika viwanja vya Shekh Amri Abeid Karume.

Kwa upande wake Askofu Dr. Masangwa alisema jamii haina budi kuunga mkono harakati za kumuenzi mama kwa kuwa ni mtu wa muhimu kwa kumhakikishia ulinzi na kuepuka vitendo vya kikatili dhidi yake.

Wanatagoane wakiwa katikati ya maandamano wakitokea Hospitali ya Mount Meru hadi uwanja wa Shekh Amria Abeid Karume baada ya kufanya usafi hospitalini hapo.

Tagoane wanaendelea kufanya tamasha hilo la siku tatu ambalo Naibu Waziri wa Afya, Dr Faustine Ndungulile atazindua uchangiaji wa damu na Naibu Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo Juliana Shonza ambaye atazindua tamasha rasmi tamasha hilo siku ya jumapili.

Like us on facebook >> Gospo Media Follow us on instagram >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Audio: Dolaa Feat. Jones Jr-Balozi

Next post

Video | Audio: Gladys Kimaro - Usimwache Mungu