Audio: Fundi wa Yesu & Baba Zedek-Kazi na Sala - Gospo Media
Connect with us

Audio: Fundi wa Yesu & Baba Zedek-Kazi na Sala

Audio

Audio: Fundi wa Yesu & Baba Zedek-Kazi na Sala

Kutoka katika kundi la Yesu Okoa Mitaa (Y.O.M) leo nawatambulisha kwako watumishi wanaomtumikia Mungu kwa mtindo wa muziki wa Gospel HipHop, Hapa namzungumzia rapa Fundi wa Yesu akiwa na Baba Zedek na huu ni wimbo wao mpya uitwao Kazi na Sala, Muziki ukiwa umetayaarishwa na kurekodiwa chini ya mikono ya prodyuza J-Dollars Beat.

Kazi na Sala ni wimbo unaotukumbusha kufanya kazi na ibada ili tusiwe wepesi wa kulaumu kwakuwa Mungu humujibu mtu maombi yake kwa wakati wake. Inawezekana wakati wa Mungu bado haujafika ili uweze kupokea majibu yako kwa yale uliyoyaomba kwake hivyo unapaswa kuendelea kusali na kufanya kazi kwa bidii ili Mungu aweze kubariki kazi za mikono yako.  Wimbo huu unashauri watu kuacha fikra za uvivu bali kufanya kazi tena kwa bidii huku tukiendelea kusubiri majibu ya maombi yetu tuliyomuomba. – alisema Fundi wa Yesu.

Kumbuka neno la Mungu kutoka katika kitabu cha Methali 10:4 Uvivu husababisha umaskini, lakini mkono wa mtu wa bidii hutajirisha.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza wimbo huu ambao ni imani yangu kuwa utakugusa na kukubariki, kumbuka #SALANAKAZI #KAZINASALA

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na rapa Fundi wa Yesu kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 713 842 636
Facebook: Fundi wa Yesu | Baba Zedek
Instagram: @fundiwayesu | @babazedek
Youtube: Baba Zedek | Fundi wa Yesu

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Audio

To Top