Audio

Audio: Sifaeli Mwabuka-Heri Lawama

Anaitwa Sifaeli Mwabuka ni mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka Tanzania na huu ni wimbo wake unaoitwa HERI LAWAMA.

Heri Lawama ni wimbo uliobeba jina la albamu yake mpya ambayo kwasasa sasa ipo sokoni akiongea na gospomedia.com Sifaeli Mwabuka amesema kupitia wimbo huu ameweza kupata baraka na kukubalika kwa kiasi kikubwa kutokana na ukweli kwamba wimbo wa Heri Lawama ni wimbo unaogusa maisha yake halisi kabisa ambayo amepitia na hivyo kuamua kuandika wimbo huu ambao hata wewe utakugusa kwa namna moja ama nyingine kwakua kila kitu kilichoandikwa na kuimbwa katika wimbo huu ni maisha halisi ambayo kwa namna moja ama nyingine wengi kati yetu tunapitia.

Sifaeli Mwabuka anasema anamshukuru Mungu kwa kukamilisha album yake hii mpya amabyo kwasasa ipo sokoni na unaweza kuipata nakala ya album hii  kwa kuwasiliana naye na kupata kusikia kile alichobarikiwa na Mungu kukugusa wewe unayehitaji faraja na msukumo wa kiroho.

Kwa mawasiliano zaidi na mwimbaji Sifaeli Mwabuka unaweza kuwasiliana naye kupitia namba zifuatazo +255719482223.

DOWNLOAD

Like us on facebook >> Gospo Media Follow us on instagram >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

PATA UJUZI TOKA KWA TONY LUVANDA 'THINK BEYOND EMPLOYMENT' BY Y.M.P

Next post

GOSPEL MUSIC VIDEO: LUCY NGAJI - NINAKUOGOPA BABA