Audio

Audio: Goodluck Gozbert – Nipe

Kutoka kwenye albamu yake iitwayo ”Shukurani” muimbaji anayeendelea vizuri katika kiwanda cha muziki wa Injili nchini Tanzania na Afrika mashariki Goodluck Gozbert ameachia wimbo wake uitwao “Nipe Kukumbuka” ukiwa ni wimbo wake wa nne kuachia kutoka kwenye albamu hiyo yenye mkusanyiko wa nyimbo nane ikiwa katika mfumo wa Audio CD.

Goodluck Gozbert ni moja kati ya waimbaji waliojizoelea umaarufu na mafanikio makubwa katika kiwanda cha muziki wa Injili nchini Tanzania na hata kuvuka mipaka ya kimataifa na kufanikiwa kujinyakulia Tuzo kadhaa za kimataifa kutokana na ubora wa kazi zake za muziki zilizobeba jumbe mbalimbali za kumsifu Mungu na kuinua mioyo ya watu.

Albamu ya Shukurani kwasasa inapatikana sokoni kupitia wakala wa Max Malipo wanaopatikana sehemu mbalimbali nchini Tanzania.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu ambao ni hakika utakubariki na kukuinua. Barikiwa!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na muimbaji Goodluck Gozbert kupitia:

Simu/WhatsApp: +255 655 212 720 au +255 654 276 560​⁠​
Facebook: Goodluck Gozbert
Instagram: @goodluckgozbert
Youtube: Goodluck Gozbert
Twitter: @goodluckgozbert
Website: www.goodluckgozbertministry.com

Like us on facebook >> Gospo Media  Follow us on instagram >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Audio: Marry Theopistor - Unatawala

Next post

Video | Audio: Moureen Boaz - Mungu Ni Mwema