Video | Audio: Waba Shadra - Simama Imara - Gospo Media
Connect with us

Video | Audio: Waba Shadra – Simama Imara

Video

Video | Audio: Waba Shadra – Simama Imara

Mwimbaji, mtayaarishaji na mwandishi wa nyimbo za Injili nchini Norway Waba Shadra ameachia video ya wimbo wake uitwao Simama Imara. Video imefanyika nchini Norway ikiwa imeongozwa na Director Dan Borge kutoka studio za ES-PRO Media Creator, Muziki ukiwa umetayaarishwa ndani ya studio za Waba Media Pro.

Simama Imara ni wimbo wa tatu kuachia kwa mwaka 2018, na ni wimbo wa mwisho kutoka kwenye albamu yake iitwayo Mji wa Amani. Wimbo huu unamgusa na kumtia moyo mtu ambaye ameingia kwenye majaribu na mapito ya aina mbalimbali, kupitia wimbo huu mwimbaji Waba Shadra anatukumbusha kusimama Imara katika Imani yetu kwa Mungu ili aweze kutawala na kuongoza maisha yetu hata pale tunapojaribiwa basi asimame kututetea kwa maana yeye ndiyo nguzo yetu.

Nina imani kuwa utabarikiwa na kuinuliwa kila utakapokuwa unasikiliza wimbo huu na Bwana Yesu akawe nguzo katika maisha yako, kuanzia sasa, Barikiwa!.

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Waba Shadra kupitia:
Simu/WhatsApp: +47 462 69 248
Facebook: Waba Shadra
Instagram: @wabashadra
Youtube: Waba Media Pro

Like us on facebook >> Gospo Media Follow us on instagram >> @gospomedia

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Video

To Top