Audio

Audio: Michael Mwampashi – Usifiwe

Mwimbaji mpya katika kiwanda cha muziki wa Injili nchini Tanzania anayefahamika kwa jina la Michael Mwampashi kwa mara ya kwanza katika mwaka 2018 ameachia wimbo wake mpya uitwao Usifiwe, Muziki ukiwa umetayarishwa na kurekodiwa ndani ya studio za Big Nation chini ya mikono ya prodyuza Gidy.

Usifiwe ni wimbo wa sifa uliobeba maneno ya shukrani na yenye kumtukuza Mungu kwa upendo wake mkuu kwetu sisi wanadamu ambao tumekombolewa kwa damu ya mwanae Yesu Kristo ambaye alikuja ulimwenguni ili mimi na wewe tupate ukombozi mpya na kuwekwa mbali na dhambi zetu.

Michael Mwampashi ni moja kati ya waimbaji wanaolelewa kihuduma na chama cha CASFETA (The Christian Ambassador Students Fellowship Tanzania) UDSM.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza wimbo huu mzuri, nikiamini kuwa utakugusa na kukubariki, Amen.

 

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Michael Mwampashi kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 765 592 479
Facebook: Michael Mwampashi
Instagram: @michael_mwampashi

Like us on facebook >> Gospo Media Follow us on instagram >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Hivi ndivyo nilivyoanza huduma na muziki mpaka nimefika Ulaya - Wabashadra

Next post

Audio: Divinely Brothers - Sitoweza