Audio: Hushai Dastan - Nisamehe - Gospo Media
Connect with us

Audio: Hushai Dastan – Nisamehe

Audio

Audio: Hushai Dastan – Nisamehe

Kutoka kiwanda cha muziki wa Injili nchini Tanzania leo nina Furaha kukutambulisha kwako mwimbaji mpya anayefahamika kwa jina la Hushai Dastan akitokea mkoani Kilimanjaro na huu ni wimbo wake wa kwanza uitwao Nisamehe ukiwa umetayaarishwa na mikono ya prodyuza Papa na kurekodiwa ndani ya studio za Biorn Production.

“Mimi nimekulia maisha ya kiutumishi kwa muda kidogo toka nimekuwa kijana mdogo…. Lakin nlivyofika chuo nikaona hali ya kiroho inabadilika lakini nilikuwa bado namuuliza Mungu kwanini… Akaniambia kuna vijana wengi kama mimi wanaogopa kutubu kwa kukiri na ninataka wewe ukiri katika wimbo utakaoimba wakati huu…
Na wakati huo nilikuwa tayari nimeutunga wimbo wenye maudhui tofauti kabisa… Hivyo Mungu akanilazimisha nitunge wimbo wa kutubu mimi kama kijana.” – Hushai Dastan

Ni hakika utaufurahia wimbo huu na kukugusa kwa namna ya pekee sana, Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu uliobeba ujumbe wa toba kwa ajili yako wewe, Barikiwa!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Hushai Dastan kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 713 920 824
Facebook: hus-shai dastan
Instagram: @husshaidastan
Twittter: @husshaidastan

Like us on facebook >> Gospo Media Follow us on instagram >> @gospomedia

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Audio

To Top