Audio: Hellen Sogia - Tanzania - Gospo Media
Connect with us

Audio: Hellen Sogia – Tanzania

Audio

Audio: Hellen Sogia – Tanzania

Mtumishi wa Mungu na mwimbaji anayefahamika kwa jina la Hellen Sogia kutoka katika kiwanda cha muziki wa Injili nchini Tanzania, Kwa mara nyingine tena ameachia wimbo wake mpya uitwao Tanzania, ikiwa ni wimbo maalumu kwa ajili ya Tanzania, Muziki huu umetayaarishwa na mikono ya prodyuza Johnson Luzzah kutoka ndani ya studio za Sogia Productions Studio.

“Katika kutafakari juu ya Nchi yangu Tanzania 🇹🇿, Nikagundua kuwa Tanzania ni Nchi ya ajabu kabisa, tuna kila kitu Tanzania, utajiri wa kutosha, tuna vitu ambavyo Nchi nyingine hawana, ni Nchi iliyowaunganisha watanzania wote kuwa kitu kimoja bila kujali dini wala kabila hiki ni kitu cha ajabu sana kwa nchi zingine katika Bara la Africa. Ndio maana halisi ya kuandika wimbo huu baada ya kuona fahari ya Tanzania, na fahari ya mimi kuwa mtanzania, NAJIVUNIA TANZANIA!.” – alisema mtumishi Hellen Sogia

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza na kupakaua wimbo huu mzuri kutoka kwa mtumishi wa Mungu Hellen na hakika utabarikiwa sana!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji(mtumishi) Hellen Sogia kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 753 351 048, +255 716 711 867
Facebook: Hellen Sogia
Instagram: @hellensogia
Youtube: Hellen Sogia

Like us on facebook >> Gospo Media  Follow us on instagram >> @gospomedia

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Audio

To Top