Connect with us

VIDEO: Steven Munugwa ft. Dorcas Jonas – Nakushukuru Yesu | Download

Video

VIDEO: Steven Munugwa ft. Dorcas Jonas – Nakushukuru Yesu | Download

VIDEO: Steven Munugwa ft. Dorcas Jonas - Nakushukuru Yesu | Download

Kutoka Tanzania kwa mara ya kwanza tunamtambulisha kwako mwimbaji wa nyimbo za Injili Steven Munugwa na hii ni video mpya ya wimbo wake unaoitwa Nakushukuru Yesu akiwa amemshirikisha mwanadada Dorcas Jonas.

“Nimeandika wimbo ikiwa ni shukrani yangu kwa Bwana Yesu kwakuwa amenitendea mengi maishani mwangu, Alinitoa mavumbini nilipokuwa maskini akanifia msalabani, ameniwezesha katika masomo yangu yaani nimepata degree bila fedha za wazazi wangu, Namshukuru Bwana Yesu kwa kumponya mama yangu ambaye alikuwa anaugua ugonjwa wa kifafa tangu akiwa Darasa la nne na hata alipotembea kwa waganga wote hakupata msaada mpaka alipokutana na Yesu mwaka 2015 ambapo aliombewa na kupokea uponyaji wake hadi sasa, Bwana amenipa uhai bure, Nilivyonavyo ni mali ya Bwana, Analinda biashara zangu n.k Naungana na kanisa kumshukuru Mungu, Neema ya Bwana i pamoja na maskini na tajiri, Amen.” – Steven Munugwa

Akiongea na GOSPO MEDIA Steven amesema kuwa wimbo huu unapatikana kwenye albamu yake ya kwanza inayoitwa KWA KISHINDO iliyo katika mfumo wa video DVD ambayo kwasasa anaisambaza yeye mwenyewe.

Karibu kutazama video ya wimbo huu na hakika utabarikiwa na kuinuliwa kupitia ushuhuda huu, Amen.

Kwa mawasiliano zaidi na Steven Munugwa wasiliana naye kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 753 682 040
Facebook: Disciple Steven Munugwa
Instagram: @disciplestevenmunugwa
Youtube: Steven Munu

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Advertisement

ZINAZOPENDWA ZAIDI

JIUNGE NASI

Jiunge na gospomedia.com ili uwe wa kwanza kupokea nyimbo za Injili kila siku kupitia barua pepe.

Join 15,013 other subscribers

To Top