Connect with us

Gospo Media

Video: Prosperous Sounds – Hakuna Kama Bwana | Download Audio MP3

Video

Video: Prosperous Sounds – Hakuna Kama Bwana | Download Audio MP3

Video: Prosperous Sounds - Hakuna Kama Bwana | Download Audio MP3

Kutoka Tanzania kwa mara ya kwanza kabisa katika mwaka 2019 tunawatambulisha kwako Prosperous Sounds na hii ni video mpya ya wimbo wao wa kwanza kuachia unaoitwa Hakuna Kama Bwana.

Prosperous Sounds ni kundi lililowakusanya vijana walioamua kumtumikia Mungu kupitia vipaji vyao uimbaji na wimbo huu ni wimbo wao wa kwanza uliowaunganisha vijana hawa na hakika kupitia ujumbe ulio katika wimbo huu utakiri kuwa umejaa upako, sifa na Ibada kwa ajili ya kuleta uamsho, kuponya, kufariji na kumtia moyo mtu aliyekata tamaa.

Prosperous Sound ni kundi lililozaliwa Disemba 2018 katika mkesha wa vijana siku ya alhamisi ndani ya kanisa la Ufufuo na Uzima Glory of Christ Tanzania Church kwa askofu Josephat Gwajima na kuanzia hapo ndipo kundi lilipoanzishwa ambapo lilianza na watu sita na mpaka sasa lina vijana wasiopungua 42 na kila mmoja akiwa anatumia kipaji alichobarikiwa kwa ajili ya ufalme wa Mungu.

Mbali na hayo yote moja kati ya viongozi wa kundi hilo Imani Nshoka alisema kuwa wakiwa kama vijana wana maono ya kuuteka ulimwengu huu wa vijana kwa kuhubiri Injili kupitia uimbaji na wana hakika kuwa watafanikiwa kuwarudisha vijana wengi kwa Yesu Kristo maana wana nguvu na uweza unaoongozwa na Roho Mtakatifu.

Tunaamini kuwa utabarikiwa na kuinuliwa kwa namna ya pekee kila wakati utakapokuwa unaitazama video hii iliyobeba habari njema kutoka kwa vijana hawa walioonesha nguvu zao kupitia vipaji vyao kwa ajili ya ufalme wa Mungu, Amen.

Kwa mawasiliano zaidi na kundi la Prosperous Sounds wasiliana na uongozi wao kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 717 133 667
Facebook: Prosperous Sounds
Instagram: @prosperous_sounds
Youtube: PROSPEROUS SOUNDS

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Video

FEATURED MUSIC

TOP 5 ON GOSPOMEDIA.COM

JIUNGE NASI

Jiunge na blog ya gospomedia.com ili uwe wa kwanza kupokea nyimbo na video mpya za muziki wa Injili kila siku kupitia barua pepe yako.

Join 13,148 other subscribers

Gospomedia.com ni blog rasmi inayokuletea nyimbo na video mpya za muziki wa Injili kilasiku kutoka ndani na nje ya Afrika.

To Top