Connect with us

Gospo Media

Audio: Miriam Patrick – Nivushe Yordani

Video

Audio: Miriam Patrick – Nivushe Yordani

Audio: Miriam Patrick - Nivushe Yordani

Miriam Patrick ni mwimbaji mpya katika anga ya muziki wa Injili akitokea jijini Dar es salaam Tanzania na huu ni wimbo wake mpya aliouachia hivi karibuni unaoitwa Nivushe Yordani.

“Nivushe Yordani ni wimbo nilioandika na kuuimba nikiwa katikati ya maombi juu ya mapito niliyokuwa napitia kwa wakati huo na hapo ndipo nilipopata ufunuo juu ya wimbo huu ambao nina imani kuwa utakugusa na kukuvusha mahali ulipo. Nafahamu huna ajira, bado hujapata mke mwema, mume mwema, magonjwa yanakusumbua na changamoto zote zinazokuzonga bado naamini na naomba wimbo huu ukuguse na kukuamsha kiroho uwe mpya kwa jina la Yesu.” – alisema Miriam

Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kusikiliza wimbo huu tukiamini kuwa utabarikiwa, Amen.

Kwa mawasiliano zaidi na Miriam Patrick wasiliana naye kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 783 458 043
Facebook: Miriam Patrick
Instagram: @miriammlanda
Youtube: Miriam Patrick

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

To Top