Connect with us

Audio: Emmanuel Estory – Tembea Nami | Listen/Download MP3

Audio

Audio: Emmanuel Estory – Tembea Nami | Listen/Download MP3

Emmanuel Estory ni mwimbaji mpya katika anga la muziki wa Injili nchini Tanzania na kwa mara ya kwanza kabisa katika mwaka 2019 ameachia wimbo wake mpya unaoitwa Tembea Nami.

Emmanuel Estory ni mwimbaji mpya katika anga la muziki wa Injili nchini Tanzania na kwa mara ya kwanza kabisa katika mwaka 2019 ameachia wimbo wake mpya unaoitwa Tembea Nami.

“Tembea Nami ni wimbo uliobeba shauku ya moyo wangu kutembea kila sekunde na YESU KRISTO wakati ninampokea YESU haya ndio yalikuwa maombi yangu kwake kutembea na yeye siku zote kama ilivyokuwa kwa mfamle Daudi na MUNGU Zaburi 17:5 “Nyayo zangu zimeshikamana na njia zako, Hatua zangu hazikuondoshwa”

Kupitia wimbo huu ni imani yangu kwamba hata wewe utaweka shauku yako kutembea na YESU kila wakati bila kujali hali gani unapitia #TembeaNaYESU Naamini utapata nguvu ya kumtegemea MUNGU na kukubali kutembea na yeye kila wakati bila kujali au kuangalia hali gani uko nayo kwasasa.” – alisema Emmanuel Estory

Muziki huu umetayaarishwa na kurekodiwa ndani ya studio za EMG Records chini ya mikono ya prodyuza Oggy Keyz

Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kusikiliza wimbo huu tukiamini kuwa utabarikiwa na kuinuliwa kwa namna ya pekee kabisa, Amen.

Kwa mawasiliano zaidi na Emmanuel Estory wasiliana naye kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 652 862 034
Facebook: Immanuel Nestory
Instagram: @emmanuelestory
Twitter: @emmanuelestory
Youtube: Emmanuel Estory

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

KALI ZA WIKI

JIUNGE NASI

Jiunge na gospomedia.com ili uwe wa kwanza kupokea nyimbo za Injili kila siku kupitia barua pepe.

Join 14,702 other subscribers

To Top