Connect with us

Gospo Media

Audio | Derick Ndonge – Kufanana Nawe | Download

Audio

Audio | Derick Ndonge – Kufanana Nawe | Download

Audio | Derick Ndonge - Kufanana Nawe | Download

Baada ya wiki chache zilizopita kuachia video ya wimbo uitwao Kwako Salama akiwa ameshirikisha Ambwene Mwasongwe kwa mara nyingine tena Derick Ndonge mwimbaji wa nyimbo za Injili nchini Tanzania ameachia wimbo wake mpya unaoitwa Kufanana Nawe.

“Kwanini kufanana nawe? Mimi natamani kufanana na Bwana Yesu kwa sababu yuko juu ya vyote ni muweza, ana upendo, hekima, maarifa, mvumilivu, mwaminifu tena mwenye huruma, ana nguvu na tabia yake kuu ni UPENDO, akipenda hupenda kweli wala habagui, hana choyo wala unafiki kikubwa zaidi aliishinda dunia na mambo yake yote. Hana ukomo wa Maisha, haugui, hachoki wala hasinzii..

Watu wengi wamekua wakitamani kufanana na watu maarufu, Matajiri, wenye vyeo, wacheza mpira maarufu, watawala wa mataifa, wazuri wa sura na maumbo hata rangi, lakini hao ni wanadamu pia huugua, huchoka, husinzia na mwanadamu ana ukomo wa maisha hata kama ukiwa na pesa kiasi gani, kuna wakati unafika utajiri wako au fedha zako au hekima yako ama elimu yako haiwezi kukusaidia chochote…

Na unaweza kutamani msaada mwingine tena zaidi ya ulivyonavyo, Unaweza kua mzuri wa sura, ukaugua sana na sura ikabadilika mwili ama umbo likabadilika kabisa ukatamani walio wazima ama ukajichukia ulivyo. Ni bora utamani kufanana na Bwana Yesu mkamilifu wa yote. Imba nami “Kufanana na Bwana Yesu”. – alisema Derick

Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kusikiliza wimbo huu mzuri wa kuabudu tukiamini kuwa utabarikiwa na kuguswa kwa namna ya pekee, Amen.

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na Derick Ndonge kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 753 661 611
Facebook: Derick Ndonge
Instagram: @derickndonge_official
Youtube: Derick Ndonge

1 Comment

1 Comment

  1. Naftal Msogoti

    July 7, 2019 at 11:55 pm

    Kazi nzuri kaka keep it up

Leave a Reply

Your email address will not be published.

To Top