Connect with us

Gospo Media

Video: Anusiata Tupevilwe – Baba Nimekuja Kwako

Video

Video: Anusiata Tupevilwe – Baba Nimekuja Kwako

Video: Anusiata Tupevilwe - Baba Nimekuja Kwako

Kutoka jijini Mwanza kwa mara ya kwanza katika mwaka 2019 leo tunamtambulisha kwako mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania Anusiata Tupevilwe na hii ni video yake ya kwanza kuachia inayoitwa Baba Nimekuja Kwako.

“Nimeandika wimbo huu katika hali ya maombi ya kumsihi Mungu arudishe amani iliyopotea katika ndoa zetu, kurudisha furaha ndani ya mioyo ya vijana wetu, kurudisha uzima katika afya zetu, kusawazisha kila aina ya shida na matatizo tuliyonayo, Kila usikilizapo wimbo huu Mungu akutendee sawa sawa na mapenzi yake.

Baba Nimekuja Kwako ni wimbo unaobeba jina la albamu yangu ya kwanza iliyo katika mfumo wa Video DVD ikiwa na mkusanyiko wa nyimbo saba zilizojaa nguvu ya Roho Mtakatifu.” – alisema Anusiata.

Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kutazama video hii tukiamini kuwa utabarikiwa na kuinuliwa kupitia ujumbe ulio katika wimbo huu, Amen.

Kwa mawasiliano zaidi wasiliana na Anusiata Tupevilwe kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 745 552 886, +255 655 761 643.
Facebook: Anusiata Tupevilwe
Instagram: @anusiatachaula
Youtube: Anusiata Tupevilwe

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Video

FEATURED MUSIC

TOP 5 ON GOSPOMEDIA.COM

JIUNGE NASI

Jiunge na blog ya gospomedia.com ili uwe wa kwanza kupokea nyimbo na video mpya za muziki wa Injili kila siku kupitia barua pepe yako.

Join 13,130 other subscribers

Gospomedia.com ni blog rasmi inayokuletea nyimbo na video mpya za muziki wa Injili kilasiku kutoka ndani na nje ya Afrika.

To Top