Video: Annoint Amani - Ni Bora Usioe - Gospo Media
Advertisements
Connect with us

Gospo Media

Video: Annoint Amani – Ni Bora Usioe

Video

Video: Annoint Amani – Ni Bora Usioe

Video: Annoint Amani - Ni Bora Usioe

Kutoka jijini Dar es salaam leo tumekusogezea video ya wimbo mpya unaoitwa Ni Bora Usioe kutoka kwa mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania al maarufu Annoint Amani.

“Huu ni wimbo ulio beba ujumbe mzito kwa kila mtu kuhusiana na mahusiano, Namna uhusiano ulivyo haribu vijana makanisani na wachungaji wameshindwa kupata hekima ya kulitatua jambo hili..wengine wanakimbia ndoa na wengine wana kimbilia ndoa, Ni bora usubiri wakati wa Mungu ili upate aliye sahihi, Na mtu aliye sahihi haimaanishi hatakuwa na mapungufu hapana ila atakuwa ni mtu ambae anaweza kuhimili ile tabia yako ambayo asiye wako asingeweza.

Kuliko kuhangaika ni bora kutulia na Yesu kwake hakuna kitu cha hasara ni faida juu ya faida maana umemtumaini aliye MUUMBAJI wa hao watu wanaoumiza kichwa wengine.

Uzinzi ni DHAMBI uwasherati ni DHAMBI usiikose MBINGU kwa ajili ya Mahusiano, MUNGU atupe hekima katika hili pia angalia unapopishana na mwenzako usijisahau wewe ni nani katika jamii, Hakikisha uhusiano wako hauondoi watenda kazi shambani mwa BWANA Barikiwa.” – Annoint Amani

Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kutazama video ya wimbo huu tukiamini kuwa utabarikiwa, Amen.

Kwa mawasiliano zaidi wasiliana na Annoint Amani kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 755 099 942
Facebook: Annoint Amani
Instagram: @annointamani
Youtube: OfficialAnnoint Amani

Advertisements
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Video

FEATURED MUSIC

Advertisements

TOP 5 ON GOSPOMEDIA.COM

Gospomedia.com ni blog ya kikristo inayokuletea nyimbo na video mpya za muziki wa Injili.

To Top