Connect with us

Gospo Media

Video: Sayuni Mrita – Yesu Amefanya

Video

Video: Sayuni Mrita – Yesu Amefanya

Kwa mara nyingine tena mwimbaji wa nyimbo za injili Tanzania, Sayuni Mrita baada ya kuachilia kibao cha “NITASHINDA TU” sasa aja na kibao kingine kikali kiendacho kwa jina la “YESU AMEFANYA”.

Video hii imeongozwa na kampuni ya Brayance Works chini ya mikono ya Director Hassan Mbangwa, Muziki ukiwa umetengenezwa na Barnabas Nason akishirikiana na Kingson na Papaa Denilson.

Ujumbe wa wimbo huu unatoka Mhubiri 9:11 “…si wenye mbio washindao katika michezo, wala si walio hodari washindao vitani, wala si wenye hekima wapatao chakula, wala si watu wa ufahamu wapatao mali, wala wenye ustadi wapatao upendeleo; lakini wakati na bahati huwapata wote”.

“Kuna wakati wa Mungu kwa kila jambo chini ya jua, Wakati wa Mungu unapofika, Mungu hubadilisha hali ya mtu na kuifanya nzuri (Mhubiri 3:11 – Mungu hufanya kila kitu kiwe kizuri kwa wakati wake…). Kwa aliyekata tamaa kuwa mambo hayaendi anavyopenda, wakati wako utafika tu na mambo yako yatabadilika na kuwa sawa. Mungu ni mwaminifu daima.” – alisema Sayuni

Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kutazama video hii njema ambayo ni hakika kuwa itakubariki kila wakati, Amen.

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma watiliana na mtumishi wa Mungu Sayuni Mrita kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 686 815 115
Facebook: Sayuni Mariki-Mrita
Instagram: @sayuni_mrita
Youtube: Sayuni Mariki-Mrita

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Video

FEATURED MUSIC

TOP 5 ON GOSPOMEDIA.COM

JIUNGE NASI

Jiunge na blog ya gospomedia.com ili uwe wa kwanza kupokea nyimbo na video mpya za muziki wa Injili kila siku kupitia barua pepe yako.

Join 13,130 other subscribers

Gospomedia.com ni blog rasmi inayokuletea nyimbo na video mpya za muziki wa Injili kilasiku kutoka ndani na nje ya Afrika.

To Top