Audio: Hellen Sogia - Wewe ni Mungu - Gospo Media
Advertisements
Connect with us

Gospo Media

Audio: Hellen Sogia – Wewe ni Mungu

Audio

Audio: Hellen Sogia – Wewe ni Mungu

Hellen Sogia ni moja kati ya waimbaji wa nyimbo za Injili wanaoendelea kufanya vizuri kila iitwapo leo kutokana na kazi anazoendelea kuziachilia ambazo mbali na kubeba ujumbe wa Ki-Mungu lakini pia zina nguvu ya Roho Mtakatifu na kwa mara ya kwanza katika mwaka 2019 ameachia wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Wewe ni Mungu.

Muziki huu umetayaarishwa na kurekodiwa ndani ya studio  za Sogia Production chini ya mikono ya prodyuza Johnson Luzzah.

“ WEWE NI MUNGU “ ni wimbo wa kuabudu, unaoelezea
– Ukuu wake Mungu
– Heshima yake Mungu
– Mungu ni Nani? Wanapojitokeza miungu wengine.
– Ni Mungu asiyefananishwa wala hastahili kulinganishwa na kitu chochote, na wala hawezi kulinganishwa na chochote kile.

Wimbo huu unamthibitisha Mungu, kuwa yeye ndio Mungu pekee, Ni Mungu wa miungu, hata walipojaribu kumweka Karibu na Dagoni, Yeye Mungu alijitibitisha kwa Dagoni, pia alijitibitisha kwa Baali, Wakati wa Eliya, alipojitokeza kama moto.

“Ilikuwa ni usiku najiandaa kulala, Nikasikia kuimba moyoni mwangu, Wewe ni Mungu, Wewe ni Mungu, hakuna kama wewe, Mungu wa miungu, niliuhifadhi na ndipo kesho yake nikaufanyia kazi studio. Karibu tumwabudu Mungu pamoja nami katika wimbo huu “ WEWE NI MUNGU”…

Mbali ya kuwa mwimbaji wa nyimbo za Injili Hellen Sogia pia ni mtumishi wa Mungu katika kufundisha na kuihubiri Injili ndani na nje ya mipaka ya Tanzania akiwa tayari ameshaandika vitabu mbalimbali vya mafundisho ya Kiroho na msingi wa Biblia.

Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kusikiliza wimbo huu mzuri wa kuabudu ambao ni hakika kuwa utakubariki, Amen.

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mtumishi Hellen Sogia kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 753 351 048, +255 716 711 867
Facebook: Hellen Sogia
Instagram: @hellensogia
Youtube: Hellen Sogia

Advertisements
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Audio

FEATURED MUSIC

Advertisements

TOP 5 ON GOSPOMEDIA.COM

Gospomedia.com ni blog ya kikristo inayokuletea nyimbo na video mpya za muziki wa Injili.

To Top