Connect with us

Gospo Media

Audio: Gift Mwamba – Maharusi

Audio

Audio: Gift Mwamba – Maharusi

Kutoka kwenye albamu yake iitwayo Uvumilivu kwa mara ya kwanza katika mwaka 2019 tumekusogezea wimbo mpya uitwao Maharusi kutoka kwa mtumishi wa Mungu anayefahamika kwa jina la Gift Mwamba.

Muziki huu umetayaarishwa na kurekodiwa ndani ya studio za Sharomu chini ya mikono ya prodyuza Eddo Montana.

“Maharusi ni wimbo uliobeba baraka nilioutunga kwa ajili ya maharusi wanaoingia kwenye Ndoa, kama tujuavyo Ndoa ni agano la maisha ya milele kati ya wanandoa walioamua kuungana pamoja katika maisha yao yote hivyo ni jambo la baraka kama tukiwaombea ili Mungu aweze kuwaongoza ili waishi kwa amani na upendo.”

Huu ni wimbo mzuri sana unaoweza kusikilizwa mahali popote pale katika kuwasindikiza maharusi huku tukifurahi pamoja tukiwaombea baraka katika maisha yao yote.

Mbali na kuachia wimbo huu Gift Mwamba ameiambia Gospomedia.com kuwa kwasasa ameshakamilisha albamu zake mbili ya kwanza ikiwa ni Uvumilivu na ya pili inaitwa Uwepo wa Mungu ambazo zote zinatarajiwa kuachiwa rasmi mwishoni mwa mwezi Machi 2019 hivyo anahitaji sapoti ya hali na mali ili aweze kuitangaza Injili kwa watu wote kupitia huduma yake ya uimbaji.

“Namshukuru Mungu kwa mwaka mwingine ambao amenibariki kuachia kazi hii kwa ajili ya wanandoa wote naamini utawabariki na kuwajaza nguvu katika maisha yao mapya ya Ndoa, Wimbo huu pia unawagusa hata wale ambao tayari wapo katika ndoa na kuwakumbusha juu ya thamani halisi ya Ndoa.” – alisema Gift

Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kusikiliza wimbo huu ambao ni hakika utakugusa na kukubariki kila wakati utakapokuwa unausikiliza, Amen.

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na Gift Mwamba kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 714 693 768 au +255 744 775 991
Facebook: Gift Mwamba
Instagram: @mwambagift
Youtube: Gift Mwamba

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Audio

FEATURED MUSIC

TOP 5 ON GOSPOMEDIA.COM

JIUNGE NASI

Jiunge na blog ya gospomedia.com ili uwe wa kwanza kupokea nyimbo na video mpya za muziki wa Injili kila siku kupitia barua pepe yako.

Join 13,130 other subscribers

Gospomedia.com ni blog rasmi inayokuletea nyimbo na video mpya za muziki wa Injili kilasiku kutoka ndani na nje ya Afrika.

To Top