Connect with us

Audio: Kiseo Pangayena – Tumaini Lisiloisha

Audio

Audio: Kiseo Pangayena – Tumaini Lisiloisha

Kutoka jijini Arusha kwa mara ya kwanza tunamtambulisha kwako mwimbaji mpya wa nyimbo za Injili anayefahamika kwa jina la Kiseo NP Pangayena na huu ni wimbo wake wa kwanza kuachia uitwao Tumaini Lisiloisha ikiwa ni wimbo unaobeba jina la albamu yake ya kwanza ikiwa katika mfumo wa Audio CD.

Muziki huu umetayaarishwa na kurekodiwa ndani ya studio za Uzao wa Kifalme Records chini ya mikono ya prodyuza Nason PP.

“Tumaini lisiloisha ni nyimbo ambayo imebeba ujumbe wa Ki-Mungu kwa wanadamu wote, hasa wale ambao inafika wakati wale waliowategemea, waliowaamini na kuwatumainia wanapotoweka katika ulimwengu wa Mwili, yaani wanapokutwa na umauti, vile ndugu wanaobaki wanapokata tamaa na kufikiri mwisho wa maisha yao umefika baada ya waliowategemea kufariki!

Ukisoma biblia, Zaburi 125:1 Wamtumainio Bwana ni kama mlima sayuni, hawatatikisika watakaa milele”
Pamoja na kuondokewa na wale ndugu waliowasaidia na kuwa msaada maishani mwao, bado lipo “TUMAINI KUU LISILOISHA” Ambalo ni Yesu pekee atabaki milele yote, naam hachagui wala habagui mtu yeyote wajane, yatima na watu wa aina yote yeye ni msaada kwao Milele.” – alisema Kiseo

Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kusikiliza wimbo huu ambao ni hakika utakubariki, Amen.

Kwa watumiaji wa tovuti bonyeza hapa chini:

[easy_media_download url=”https://gospomedia.com/wp-content/uploads/2018/12/Kiseo-Pangayena-Tumaini-Lisiloisha.mp3″ text=”Download Audio” force_dl=”1″]

Kwa watumiaji wa App bonyeza hapa chini:
Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Kiseo kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 765 351 001
Facebook: Kiseo Pangeyena
Instagram: @kiseopangeyena

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Audio

TOP 5 ON GOSPOMEDIA.COM

JIUNGE NASI

Jiunge na jukwaa la gospomedia.com ili uwe wa kwanza kupokea nyimbo na video mpya za muziki wa Injili kila siku kupitia barua pepe.

Join 14,056 other subscribers

Akawaambia, Nendeni ulimwenguni kote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.Marko 16:15 – 16

To Top