Connect with us

Video | Audio: Hellen Sogia – Umetukuka

Audio

Video | Audio: Hellen Sogia – Umetukuka

Kutoka jijini Dar es salaam kwa mara nyingine tena tumekusogezea video ya wimbo mpya uitwao Umetukuka kutoka kwa mwimbaji na mtumishi wa Mungu Hellen Sogia akiwa amemshirikisha Johnson Luzzah.

Video hii imeongozwa na director Japhet, Muziki ukiwa umetayaarishwa na kurekodiwa ndani ya studio  za Sogia Production chini ya mikono ya prodyuza Johnson Luzzah.

“Umetukuka ni wa kuabudu, niliopewa nikiwa nimetulia uweponi mwake Bwana, na ndipo nikiwa nimeibusu miguu yake, nikaona ni furaha ya ajabu moyoni kwangu, ndipo nikaimba, uweponi mwako ndipo kwenye furaha yangu.” – alisema mtumishi Hellen Sogia

Huu ni wimbo unaobeba jina la la albamu yake ya tano iliyosheheni nyimbo mbalimbali za kuabudu ikiwa katika mfumo wa Audio CD na Video (DVD).

Mbali ya kuwa mwimbaji wa nyimbo za Injili Hellen Sogia pia ni mtumishi wa Mungu katika kufundisha na kuihubiri Injili ndani na nje ya mipaka ya Tanzania akiwa tayari ameshaandika vitabu mbalimbali vya mafundisho ya Biblia.

Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kutazama video hii ambayo tunaamini itakubariki na kukuinua siku zote, Barikiwa.

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mtumishi Hellen Sogia kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 753 351 048, +255 716 711 867
Facebook: Hellen Sogia
Instagram: @hellensogia
Youtube: Hellen Sogia

Like us on facebook >> Gospo Media  Follow us on instagram >> @gospomedia

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

KALI ZA WIKI

JIUNGE NASI

Jiunge na gospomedia.com ili uwe wa kwanza kupokea nyimbo za Injili kila siku kupitia barua pepe.

Join 14,785 other subscribers

To Top