Audio: Delta Music Feat. Chombaa, Akali, Pradeta & Kodo - MV Nyerere - Gospo Media
Advertisements
Connect with us

Gospo Media

Audio: Delta Music Feat. Chombaa, Akali, Pradeta & Kodo – MV Nyerere

Audio

Audio: Delta Music Feat. Chombaa, Akali, Pradeta & Kodo – MV Nyerere

Tukiwa katika huzuni kubwa kwa taifa baada ya ajali ya kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere iliyotokea tarehe 20 September 2018 na kupoteza maisha ya watu zaidi ya 200, Umoja wa wasanii nchini Tanzania wakishirikiana na Studio za Delta Music wameachia wimbo wa maombolezo uitwao MV Nyerere ikiwa ni sehemu ya kutoa faraja kwa ndugu, jamaa na watanzania wote tuliofikwa na msiba huu mkubwa.

Mv Nyerere ilipinduka karibu na fukwe za Ukara ikiwa safarini kutoka Bugorora.

Rais wa Tanzania amenukuliwa na msemaji wa serikali Gerson msigwa akisema ameshtushwa sana na mkasa wa kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere.

Amenukuliwa:

Nimeshtushwa na kusikitishwa sana na ajali ya MV Nyerere, nawapa pole wote waliopoteza jamaa zao na nawaombea wote walionusurika kupona haraka, kwa wakati huu nawaomba tutulie wakati juhudi za uokoaji zinaendelea

Dkt John Magufuli – Rais wa Tanzania

Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kusikiliza wimbo huu kuungana na watanzania wote katika kuomba pamoja kwa ajili ya ndugu zetu waliopoteza maisha yao katika ajali hiyo. Bwana ametoa, Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.

 

Download Audio

Like us on facebook >> Gospo Media Follow us on instagram >> @gospomedia

Advertisements
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Audio

FEATURED MUSIC

Advertisements

TOP 5 ON GOSPOMEDIA.COM

Gospomedia.com ni blog ya kikristo inayokuletea nyimbo na video mpya za muziki wa Injili.

To Top