Connect with us

Gospo Media

Video | Audio: Nsiandumi – Ibada

Audio

Video | Audio: Nsiandumi – Ibada

Baada ya kimya cha muda wa takribani mwaka mmoja toka alipoachia wimbo wake uitwao Mungu Mmoja mwaka 2017 mwimbaji anayeendelea kufanya vizuri ndani ya nje ya mipaka ya Tanzania maarufu kama Nsiandumi kwa mara ya kwanza katika mwaka 2018 ameachia video ya wimbo wake mpya iitwayo Ibada.

Video hii imeongozwa na director Moses Londo kutoka studio za Kynetic, Muziki ukiwa umetaayarishwa na kurekodiwa chini ya mikono ya prodyuza Taz Goemi kutoka ndani ya studio za Fishers Records.

“Wimbo huu unamlenga mtu anayetamani kumfanyia MUNGU Ibada katika roho na kweli. Tunapomuabudu Mungu, tunapokuwa katika uwepo wake, Yeye huwa anatuhudumia pia. Katika uwepo wake kuna Uhuru, kuna kupona, kufunguliwa, kuta na vizuizi huvunjwa na kuharibiwa, minyororo pia hukatika. Kuna amani katika uwepo wa MUNGU hivyo mtu atakayeamua kumuabudu Mungu kutumia wimbo huu ni hakika atabarikiwa!

Mbali na huduma ya uimbaji Nsiandumi ni mtumishi wa Mungu akiwa ni Mchungaji kiongozi wa kanisa la Bread of Life Church linalopatikana Jengo la LAPF building, ghorofa ya 14 jijini Dar es salaam, Tanzania.

Ni hakika utabarikiwa na kuinuliwa kupitia video ya wimbo huu wa Ibada utakaokuongoza vyema siku zote, Karibu kutazama!

Nunua wimbo huu kupitia:

Amazon Music – https://amzn.to/2OOKxRm
Apple Music – https://apple.co/2PpTl0X
Deezer – https://bit.ly/2N3NNHY
iTunes – https://apple.co/2PqouBu
Napster – https://bit.ly/2MswROW
Spotify – https://spoti.fi/2PqZaeG
Tidal – https://bit.ly/2nTvhqX

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mtumishi wa Mungu Nsiandumi kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 783 454 463
Facebook: Nsiandumi
Instagram: @nsiandumi
Twittter: @nsiandumi
Youtube: Nsiandumi Ndossi

Like us on facebook >> Gospo Media Follow us on instagram >> @gospomedia

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Audio

FEATURED MUSIC

TOP 5 ON GOSPOMEDIA.COM

JIUNGE NASI

Jiunge na blog ya gospomedia.com ili uwe wa kwanza kupokea nyimbo na video mpya za muziki wa Injili kila siku kupitia barua pepe yako.

Join 13,130 other subscribers

Gospomedia.com ni blog rasmi inayokuletea nyimbo na video mpya za muziki wa Injili kilasiku kutoka ndani na nje ya Afrika.

To Top