Connect with us

Audio: Hellen Sogia – Calvary

Audio

Audio: Hellen Sogia – Calvary

Mwimbaji na mtumishi wa Mungu Hellen Sogia, Kwa mara nyingine tena ameachia wimbo wake mpya wa Ibada uitwao Calvary, Muziki huu umetayaarishwa na kurekodiwa ndani ya studio za Sogia Studio Productions, chini ya mikono ya prodyuza Johnson Luzzah.

Calvary ni wimbo wa Ibada unaokiri ushindi na ukombozi wetu baada ya kumwagika kwa damu ya Bwana wetu Yesu Kristo pale Calvary(Golgotha). Ni wimbo unaotukumbusha juu ya mateso, damu na msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo ambaye alibeba laana zetu, dhambi zetu, magonjwa yetu na kila aina ya vifungo vyetu ambavyo vyote vilivunjwa na kufutwa, amebadilisha maisha yetu, ametutakasa na kuwa viumbe wapya.

Wimbo huu uguse moyo wako ili upate kutambua thamani ya damu ya Yesu iliyomwagika msalabani kwa ajili ya watu wote duniani.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza wimbo huu ambao ni imani yangu kuwa utabarikiwa!

 

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mtumishi Hellen Sogia kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 753 351 048 au +255 716 711 867
Facebook: Hellen Sogia
Instagram: @hellensogia
Youtube: Hellen Sogia

Like us on facebook >> Gospo Media  Follow us on instagram >> @gospomedia

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

KALI ZA WIKI

JIUNGE NASI

Jiunge na gospomedia.com ili uwe wa kwanza kupokea nyimbo za Injili kila siku kupitia barua pepe.

Join 14,697 other subscribers

To Top