Connect with us

Audio: Juliana Mathias – Pendo la Kweli

Audio

Audio: Juliana Mathias – Pendo la Kweli

Baada ya kufanya vizuri sana mwaka 2017 kupitia wimbo wake uitwao Tangu Nikujue Yesu mwimbaji wa nyimbo za Injili anayefahamika kama Juliana Mathias kutoka jijini Dar es salaam kwa mara ya kwanza katika mwaka 2018 ameachia wimbo wake mzuri wa Ibada uitwao Pendo la Kweli, Muziki huu umetayaarishwa na kurekodiwa ndani ya studio za Ebenezer chini ya mikono ya prodyuza Dan.

“Pendo la Kweli ni wimbo ambao nimeimba kwa ajili ya kumshukuru Mungu, amekuwa pamoja na mimi na kunipigania nyakati tofauti tofauti.. Nafahamu kuna nyakati binadamu wanaweza kuniacha lakini Mungu amekuwa na mimi bila kuniacha hivyo nimeona upendo wake mkuu kwangu na hakika ni upendo wa wa ajabu sana…

Nakumbuka nilipita katika jaribu la maradhi yaliyonisumbua sana sana, Lakini bado Mungu akaniponya na nikasimama na kutembea kabisa wakati nilikuwa siwezi hata kunyanyua mguu wangu, Hivyo Mungu amekuwa pamoja na mimi kila wakati bila kuchoka na hii ndio sababu iliyonipa msukumo wa kuandika wimbo huu wa kumshukuru Mungu kwa aliyonitendea katika maisha yangu.

Barikiwa wewe ambaye utaguswa na wimbo huu kila wakati utakapokuwa unasikiliza nakuombea Baraka kwa Mungu nawe upate kuishi ndani upendo wake mkuu, Ameen!” – Juliana alisema

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza wimbo huu nikiamini kuwa utakugusa na kukupa nguvu ya imani kila siku, Barikiwa!

 

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Juliana Mathias kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 656 851 380
Instagram: @officialjuliana_mathias

Like us on facebook >> Gospo Media Follow us on instagram >> @gospomedia

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

KALI ZA WIKI

JIUNGE NASI

Jiunge na gospomedia.com ili uwe wa kwanza kupokea nyimbo za Injili kila siku kupitia barua pepe.

Join 14,697 other subscribers

To Top