Video | Audio: Valentino Mhongole - Mrudie Muumba - Gospo Media
Advertisements
Connect with us

Gospo Media

Video | Audio: Valentino Mhongole – Mrudie Muumba

Audio

Video | Audio: Valentino Mhongole – Mrudie Muumba

Kutoka mkoani Iringa leo kwa mara ya kwanza nimekuletea video ya wimbo uitwao Mrudie Muumba kutoka kwa kwa mwimbaji mpya katika huduma ya muziki wa Injili nchini Tanzania, Video hii imeongozwa na director Romalio na Muziki ukiwa umetayaarishwa na kurekodiwa ndani ya studio za KMP Records chini ya mikono ya prodyuza Robinson.

Mrudie Muumba ni wimbo wa nne unaopatikana kwenye albamu yake ya kwanza iitwayo Ulivyo wa Ajabu yenye mkusanyiko wa nyimbo saba ikiwa katika mfumo wa Audio CD.

Mrudie Muumba ni wimbo uliobeba ujumbe wa kumkumbusha mwanadamu juu ya umuhimu wa kutubu na kumrudia Mungu ikiwa ni alama ya kukiri na unyenyekevu mbele za Mungu, Inawezekana wewe ambaye unasikiliza wimbo huu wakati huu bado unaishi maisha ya dhambi ambazo ni hakika zimekutenga mbali na Mungu, Hivyo wimbo huu uwe kengele itakayokugusa na kubadilisha maisha yako kuanzia sasa.

Luka 15:7
Kadhalika nawaambieni, ndivyo kutakavyokuwa na furaha mbinguni kwa ajili ya kutubu kwa mwenye dhambi mmoja, kuliko kwa ajili ya watu tisini na tisa wanaojiona kuwa wema, wasiohitaji kutubu.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kutazama video hii ambayo ni imani yangu kuwa itakugusa na kubadilisha maisha yako. #MrudieMuumba

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Valentino Mhongole kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 755 978 976
Facebook: Valentino Mhongole
Email: mhongolev@gmail.com

Like us on facebook >> Gospo Media Follow us on instagram >> @gospomedia

Advertisements
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Audio

FEATURED MUSIC

Advertisements

TOP 5 ON GOSPOMEDIA.COM

Gospomedia.com ni blog ya kikristo inayokuletea nyimbo na video mpya za muziki wa Injili.

To Top