Video | Audio: Theofrida Gervas - Kama Siyo Wewe - Gospo Media
Advertisements
Connect with us

Gospo Media

Video | Audio: Theofrida Gervas – Kama Siyo Wewe

Audio

Video | Audio: Theofrida Gervas – Kama Siyo Wewe

Baada ya kufanya vizuri kupitia video ya wimbo wake uitwao Wewe ni Mwema, Mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka jijini Dar es salaam Tanzania Theofrida Gervas kwa mara nyingine tena ameachia video ya wimbo wake mpya uitwao “Kama Siyo Wewe”, Video hii imeongozwa na director Jackson Joachim kutoka studio za Blessing na Muziki ukiwa umetayaarishwa na kurekodiwa ndani ya studio za Pax chini mikono ya prodyuza Timothy.

“Shalom mpendwa! KAMA SIYO WEWE ni wimbo ambao niliuandika mwaka 2012 baada ya kupitia changamoto kubwa mno ambazo kibinadamu ulikuwa mwisho wa tumaini la ndoto zangu, ashukuriwe Mungu aliyemaliza changamoto hiyo na kunipa furaha ya maisha isiyokoma na sasa nakiri kuwa KAMA SIYO YEYE nisingekuwa hapa leo hii. Nakutia moyo kupitia wimbo huu, Mungu akuvushe katika hilo unalopitia, sijui namna gani linakuumiza ninachojua mimi ni NGUVU YA MUNGU itakayokuvusha hapo uwe shule, nyumbani, mtaani, ofisini au utumwani YESU atabadilisha hali yako Usiogope! Kama Siyo Yesu, Israel asimame na Aseme! Karibu utazame video hii na usisahau kusubscribe na kuwashirikisha kwa wale uwapendao.” – alisema mwimbaji Theofrida

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kutazama video hii nikiamini kuwa wimbo huu utakugusa na kukubariki kwa namna ya tofauti sana.

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Theofrida Gervas kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 655 605 377
Facebook: Theofrida Gervas
Instagram: @theofridagervasofficialtz
Youtube: theofrida gervas

Like us on facebook >> GOSPO MEDIA  Follow us on instagram >> @gospomedia

Advertisements
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Audio

FEATURED MUSIC

Advertisements

TOP 5 ON GOSPOMEDIA.COM

Gospomedia.com ni blog ya kikristo inayokuletea nyimbo na video mpya za muziki wa Injili.

To Top