Connect with us

Gospo Media

Video | Audio: Richie kisukuli – Nahitaji

Audio

Video | Audio: Richie kisukuli – Nahitaji

Kutoka jijini Dar es salaam kwa mara ya kwanza namtambulisha kwako mwimbaji mwimbaji mpya katika kiwanda cha muziki wa Injili nchini Tanzania anayefahamika kwa jina la Richie Kisukuli na hii ni video ya wimbo wake wa kwanza kwa mwaka 2018 uitwao Nahitaji, Video hii imeongozwa na director Hanzo kutoka studio za Paradise vision production na Muziki ukiwa umetayaarishwa na kurekodiwa ndani ya studio za Pluto 6 Records chini ya mikono ya prodyuza Black Culture na Sajo.

“NAHITAJI ni wimbo unaotueleza kwamba, Katika kila hali usikate tamaa wala kufa imani hata kulaumu/kukufuru ukuu wa Mungu nakufanya mambo yasipo mpendeza. Mungu wetu ni mwaminifu hawai wala hachelewi, ila hujibu kwa wakati. Endelea kusubiri huku ukimuomba akutendee mambo makuu maishani mwako, Mtumikie yeye katika roho na kweli naye atakufungulia milango ya majibu. AMEN.” – alisema Richie Kisukuli

Nina imani kubwa kuwa wimbo huu utakugusa na kukuinua katika viwango vikubwa sana kiimani na kukupa matumaini mapya kwa yale ambayo unapitia kwasasa yawezekana una fulani ambayo unaona ni nzito kuitatua katika mtazamo wa kimwili lakini kwa ukiamini katika Mungu mambo yote yanawezekana.  Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kuitazama video hii na kusikiliza wimbo huu na Mungu akubariki katika viwango vingine.

[easy_media_download url=”https://gospomedia.com/wp-content/uploads/2018/06/Richie-Kisukuli-Nahitaji.mp3″ text=”Download Audio” force_dl=”1″]

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Richie Kisukuli kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 746 468 922
Instagram: @richiekisukuli
Youtube: Richie Kisukuli

Like us on facebook >> Gospo Media Follow us on instagram >> @gospomedia

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Audio

FEATURED MUSIC

TOP 5 ON GOSPOMEDIA.COM

JIUNGE NASI

Jiunge na blog ya gospomedia.com ili uwe wa kwanza kupokea nyimbo na video mpya za muziki wa Injili kila siku kupitia barua pepe yako.

Join 13,147 other subscribers

Gospomedia.com ni blog rasmi inayokuletea nyimbo na video mpya za muziki wa Injili kilasiku kutoka ndani na nje ya Afrika.

To Top