Connect with us

Gospo Media

Audio: Divinely Brothers – Sitoweza

Audio

Audio: Divinely Brothers – Sitoweza

Kutoka katika kiwanda cha muziki wa Injili nchini Tanzania leo kwa mara ya kwanza nawatambulisha kwako kundi jipya la waimbaji wa nyimbo za Injili linalofahamika kwa jina la Divinely Brothers na huu ni wimbo wao wa kwanza kwa mwaka 2018 uitwao “Sitoweza” ukiwa umetayaarishwa na kurekodiwa ndani ya studio za Andrew Music chini ya mikono ya prodyuza Andrew.

“Sitoweza ni wimbo unaovuta ukiri juu ya uweza wa Mungu juu ya Maisha yetu, ya kwamba lolote tufanyalo ni kwasababu ni Mungu tu ameruhusu na si kwa uweza wa akili zetu.. Yohana 15:6 Mtu yeyote asipokaa ndani yangu hutupwa nje kama tawi litupwalo nje hata likakauka. Watu huliokota tawi la namna hiyo na kulitupa motoni liungue.” – walisema Divinely Brothers

Divinely Brother ni kundi linalowaunganisha vijana wawili akiwemo Prosper na Raphael wakiwa ni ndugu ambao wameamua kumtumia Mungu kwa njia ya uimbaji na huu ukiwa ni utambulisho wao wa kwanza na wameahidi kuendelea kuachia kazi nyingine zaidi ambazo wanaamini zitawabariki na kuwagusa watu wengi zaidi, ikiwa ndio kusudi lao kuu katika kuitangaza Injili ya Yesu Kristo.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza wimbo huu mzuri, Nikiamini kuwa utakubariki na kukuinua. Bwana Yesu asifiwe!

 

[easy_media_download url=”https://gospomedia.com/wp-content/uploads/2018/06/Divinely-Brothers-Sitoweza.mp3″ text=”Download Audio” force_dl=”1″]

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na kundi la Divinely Brothers kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 653 096326, +255 719 009 734
Facebook: Divinely Brothers
Instagram: @divinelybrothers
Youtube: Divinely Brothers

Like us on facebook >> Gospo Media Follow us on instagram >> @gospomedia

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Audio

FEATURED MUSIC

TOP 5 ON GOSPOMEDIA.COM

JIUNGE NASI

Jiunge na blog ya gospomedia.com ili uwe wa kwanza kupokea nyimbo na video mpya za muziki wa Injili kila siku kupitia barua pepe yako.

Join 13,130 other subscribers

Gospomedia.com ni blog rasmi inayokuletea nyimbo na video mpya za muziki wa Injili kilasiku kutoka ndani na nje ya Afrika.

To Top