Connect with us

Gospo Media

Audio: Dona JR Feat. Miriam Jackson & Prophet Bashando – Do it Now

Audio

Audio: Dona JR Feat. Miriam Jackson & Prophet Bashando – Do it Now

Moja ya Rapa mahiri wanaoendelea kufanya vizuri katika kiwanda cha muziki wa Injili Tanzania ni pamoja na Dona JR ambaye ameonekana kuendelea kuachia nyimbo zenye mguso na kutoa matumaini kwa watu wengi hii ni baada ya kuachia wimbo wake uitwao “Narudi” mwezi Februari 2018 akiwa amemshirikisha mwanadada Rebecca na sasa  ameachia wimbo wake mpya kabisa uitwao DO IT NOW akiwa amemshirikisha mwanadada Miriam Jackson pamoja na rapa mahiri anayefahamika kama Prophet Bashando, Muziki huu umetayarishwa na kurekodiwa ndani ya studio za Enzi Records chini ya mikono ya prodyuza Amzy.

“DO IT NOW ni wimbo ambao unasisitiza watu hasa vijana kutokata tamaa na kufanya vitu bila kupoteza muda (without delaying) Kama neno la Mungu linavyotuambia kuwa WAKATI WA WOKOVU NI SASA na kulingana na asili ya maisha yetu kwa sasa umri wa kuishi umepungua hivyo tunatakiwa tufanye kazi ya Bwana kama mwisho wa dunia ni kesho (yaani wakati ambao Masihi anakuja kulichukua kanisa) kwa hiyo ukipata nafasi ya kufanya kitu kwa ajili ya Mungu fanya hadi kile kitu unachokifanya kijue kwamba wewe ndo umeagizwa na Mungu ukifanye (MAKE THE PERFECT FOR EVERY OPPORTUNITY) Fanya sasa #DOITNOW. ” – Alisema Dona.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza wimbo huu nikiamini kuwa utakwenda kubadilisha maisha yako kuanzia sasa. DO IT NOW !!

 

[easy_media_download url=”https://gospomedia.com/wp-content/uploads/2018/06/Dona-JR-Feat.-Miriam-Jackson-Prophet-Bashando-DO-IT-NOW.mp3″ text=”Download Audio” force_dl=”1″]

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na rapa Dona JR kupitia:-
Simu/WhatsApp: +255 746 083 735, +255 713 02 44 55
Facebook: Donanciano Van Joseph
Instagram: @255dona
Twitter: @255dona
Youtube: DONA Jesus Rapper

Like us on facebook >> Gospo Media Follow us on instagram >> @gospomedia

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Audio

FEATURED MUSIC

TOP 5 ON GOSPOMEDIA.COM

JIUNGE NASI

Jiunge na blog ya gospomedia.com ili uwe wa kwanza kupokea nyimbo na video mpya za muziki wa Injili kila siku kupitia barua pepe yako.

Join 13,131 other subscribers

Gospomedia.com ni blog rasmi inayokuletea nyimbo na video mpya za muziki wa Injili kilasiku kutoka ndani na nje ya Afrika.

To Top