Video | Audio: Shadrack Robert - Siyabonga Jesu - Gospo Media
Advertisements
Connect with us

Gospo Media

Video | Audio: Shadrack Robert – Siyabonga Jesu

Video

Video | Audio: Shadrack Robert – Siyabonga Jesu

Leo ikiwa ni siku ya Pasaka iliyojaa furaha na shangwe katika kuenzi kufufuka kwa Bwana wetu Yesu Kristo kwa mara nyingine tena leo kupitia tovuti yako pendwa nimekusogezea video ya wimbo mpya uitwao “Siyabonga Jesu” ikiwa ni kazi yake ya pili kuachia kwa mwaka 2018 kutoka kwenye lebo yake iitwayo Asheengai Music, video hii imeongozwa na director Decha na muziki ukiwa umetayaarishwa na mikono ya prodyuza Samtimber kutoka ndani ya studio za Fnouk Production, Arusha.

“Siyabonga Jesu ni neno la lugha ya Kizulu inayozungumzwa nchini Afrika Kusini ikiwa na maana ya Asante Yesu. Huu ni wimbo wa kumrudishia Bwana Yesu Sifa na utukufu kwa maana kwa kufufuka kwake sisi tumepata wokovu na utakaso, kila mmoja sasa kwa nafasi yake amtafakari Mungu huku akishangilia kwa furaha juu kufufuka kwa Bwana wetu Yesu Kristo ikiwa ni alama kuu ya upendo wake kwetu sisi wanadamu.” – Alisema Shadrack

Shadrack Robert Moja kati ya waimbaji wanaofanya vizuri katika kiwanda cha muziki wa Injili nchini Tanzania  akiwa anaonekana kupiga hatua kimataifa kwa kazi ambazo anaendelea kuziachia siku hadi siku.

Ni hakika utabarikiwa na kuifurahia video hii baada ya kuitazama, nina imani kuwa Mungu atakupa nafasi ya ushindi juu ya vita unayopigana kwa maana mfalme wetu Yu Hai, Ameen.

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Shadrack Robert kupitia
Simu/WhatsApp: +255 767 897 260
Facebook: Shadrack Robert
Instagram: @shadrackrobert
YouTube: Shadrack Robert
Email: thisisshadrack@gmail.com

Like us on facebook >> GOSPO MEDIA  Follow us on instagram >> @gospomedia

Advertisements

More in Video

FEATURED MUSIC

Advertisements

TOP 5 ON GOSPOMEDIA.COM

Gospomedia.com ni blog ya kikristo inayokuletea nyimbo na video mpya za muziki wa Injili.

To Top