Video | Audio: Shadrack Robert - Wimbo - Gospo Media
Advertisements
Connect with us

Gospo Media

Video | Audio: Shadrack Robert – Wimbo

Video

Video | Audio: Shadrack Robert – Wimbo

Moja kati ya waimbaji wanaoendelea kufanya vizuri katika kiwanda cha muziki wa Injili Tanzania hutaacha kumgusa mwimbaji Shadrack Robert kutoka jijini Arusha akiwa ni moja kati ya mwimbaji mwenye ari na nguvu ya kumtumikia Mungu kwa njia ya muziki wa Injili, akiwa tayari ameshafanya vizuri kupitia nyimbo na video zake ambazo ameshaziachia kama vile Elshadai, Nijaze Roho, Malaika, I want to know You, Siyabonga, Mungu Nilinde, Usiyelala na Nikuimbie ambapo nyimbo hizi zote zimekuwa na mguso wa kipekee kutokana na vile zinavyoendelea kuwabariki watu wengi kwa namna tofauti.

Leo kupitia tovuti yako pendwa nimekuletea video yake mpya iitwayo Wimbo ikiwa ni kazi yake ya kwanza kwa mwaka 2018 kutoka kwenye lebo yake iitwayo Asheengai Music, ikiwa imeongozwa na director Decha na muziki ukiwa umetayaarishwa na mikono ya prodyuza Samtimber kutoka ndani ya studio za Fnouk Production.

Huu ni wimbo wa Sifa unaoelezea utukufu wa Bwana wetu Yesu Kristo kwa yale ambayo ameyatenda katika maisha yetu na kudhihirisha upendo wake wa kweli kwetu hata sasa bado amekuwa akitutendea miujiza isiyoweza kuelezeka ndio maana leo tunaimba WIMBO huu kurudisha shukrani na sifa kwakwe na watu wajue kuwa ametenda, Ameen.

Huu ni wimbo wenye mchanganiko wa vionjo vya muziki wa kiafrika utakaokufanya upate kuufurahia, kusikiliza na kutazama video hii ambayo imetayaarishwa katika ubunifu wa kipekee zaidi.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kutazama video hii na kupakua wimbo huu ambao nina hakika kuwa utaufurahia na kubarikiwa zaidi kila utakapokuwa unasikiliza na kuitazama video hii, Ameen.

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Shadrack Robert kupitia
Simu/WhatsApp: +255 767 897 260
Facebook: Shadrack Robert
Instagram: @shadrackrobert
YouTube: Shadrack Robert
Email: thisisshadrack@gmail.com

Like us on facebook >> GOSPO MEDIA  Follow us on instagram >> @gospomedia

Advertisements

More in Video

FEATURED MUSIC

Advertisements

TOP 5 ON GOSPOMEDIA.COM

Gospomedia.com ni blog ya kikristo inayokuletea nyimbo na video mpya za muziki wa Injili.

To Top